Tuesday, September 8, 2009

RECIPE YA WIKI HII.......PILAU LA KUKU


Nafahamu kuwa kila mtu anayo namna yake ya kupika, ila recipe ninazo toa humu ni namna vile ninavyo pika mimi na huwa kinatoka kitamu tu na walaji wana enjoy

Jinsi ya kupika pilau la kuku/ au nyama nyingine yoyote unayoipenda wewe.
Ila kama ni la kuku atapendeza zaidi akiwa ni kuku wa kienyeji.

Ukishamkata kuku/nyama ukaosha vizuri, unaweka chumvi na ndimu.
Unabandika jikoni viive bila kuongeza maji, ikishakauka maji maji yote unakaanga mpaka iwe brown, au kama hupendi wa kukauka sana unakaanga kidogo tu
Halafu unahifadhi sehemu unasubiri ijichuje mafuta
Kumbuka pia kukaanga na viazi mbatata navyo uvihifadhi pembeni

Unaosha mchele unachuja maji yote kisha unauhifadhi kwenye chombo kikavu.
Pembeni unakuwa umekata kata viungo, Chumvi, Vitunguu, Nyanya ya ku blend, Karot ndogo ndogo ikibidi zikate kwa mshine sio kwa mkono,
Garlic ya kutosha pia uwe ume blend au wengine hupenda kuponda kwenye kinu kwa imani kuwa haitapoteza ladha yake ya asilia.
Mimi pia napenda kutwanga kwenye kinu badala ya kutumia blender.
Viungo vya Pilau vilivyo changanywa kwa pamoja, mdala sini (vile vimbao mbao)

Chemsha maji ya moto kwenye sufuria tofauti na utakalopikia pilau yako.

Baada ya kuwa umesha andaa vitu vyote hivyo unaanza kama ifuatavyo

Weka mafuta kwenye sufuria mpaka yachemke kabisa
Weka vitunguu, kaanga kidogo kisha ongeza karot. Acha vichemkie halafu ongeza nyanya ya kusagwa.
Funikia tena vichemke kidogo halafu weka vitunguu thaumu vilivyo sagwa, Ongezea na viungo vya pilau halafu acha tena kidogo.

Ukiona vimechanganyika vema, weka mchele, chumvi pamoja na maji kidogo.
Maji lazima yawe ya moto, jitahidi kuangalia kipimo cha maji kisizidi usije kutoa bokoboko.

Funikia huku ukiwa umepunguza moto ili kisiungue kwa chini.
Baada ya dakika kama 20 pilau lako litakuwa limewiva.
Unatayarisha chombo kikubwa unamwaga ule wali wote kisha unachanganya na Kuku/nyama pamoja na vile viazi ulivokuwa umevikaanga mwanzo. unafunika kwa dakika kama 5-10 ili mvuke wa harufu ya viungo uchanganyike na kuku/nyama na viazi.

Baada ya hapo unaweza kupakua na kuweka mezani na itakuwa tayari kwa kuliwa.
Usisahau kachumbari ya kiswahili kwa pembeni, ya Nyanya, Vitunguu na Matango au Chachandu

Enjoy

35 comments:

Jacque said...

Asante mamie kwa pishi la pilau na recipe zake!

Anonymous said...

Mama Gardner Mimi like to call u brown sugar no coffee no Tea nakuona una ka Red Wine hapo kwa afya ,Najua unapenda kupika like me Sasa nikupe Pilau la Viungo vya kuchemsha mpenzy sawaaaaaa Nunua Abdala Sin,Bizari nyembamba(Ile kam Mchele),Iliki,Karafuu etc etc ,Au Sema viungo vizima visivyopondwa sokoni halafu ukishataarisha mahitaji yako kam awali ukikaanga vitunguu maji,swaumu,tangawizi ,karoti etc etc tia mchele sawa badala ya wakati ule si ulikuwa watia viungo vyako sasa wakati wa kutia maji ndo waweka maji yale ya viungo ulivyochemsha unaongezea na soup ya kuku au nyama.Ila sio mpenzy uchemshe viungo na maji lundo nono kidogo kama glass mbili hivi za maji vichemke mpk vitoe harufu ndo waipua sasa wafanya kam kawaida yako sawaaaa Kaflower Jide ,Ni taamu mpenz jaribu unipe majibu

Anonymous said...

Manka naomba niwe mgeni wako siku moja.

JO said...

i always lov pilau la kuku sema sasa nimebakia kupika la nyama tu nilihisi la kuku sio tamu jinsi liko linavovutia isee napika langu asante kwa recipe...jide mimi hupika sana tambi lakini pishi langu huwa ni lile la kuzipika kwa maji yakisha kauka unageuza geuka mpaka ikauke isionekane maji wala mafuta mengi sasa nilienda matembezini huko nakaletewa tambi jamani zina viungo mbalimbali zinavutia na zimepikwa kwa kukaangwa na maini unawza nipatia recipe yake? napenda kupika na huwa nasoma nyingi hapa

chib said...

Umenikumbusha sana nyumbani. Huku sibahatishi pilau la nguvu kama hilo

Anonymous said...

napenda watu watundu kama wewe,mwanamke kupika.

Jide said...

J.O tambi za maini hata mimi nilikutana nazo Protea hotel nikaomba mpaka recipe maana nilishindwa kujizuia, next week nakupa wangu usijali.

Anonymous said...

Manka nitakupataje natamani tambi za maini.

JO said...

thanx sana naisubiri ni tamu aisee

Anonymous said...

duh.. hongera jide, sasa kwa style hii uncle gardner ataacha kupata kitambi kweli? hahahaha.. mke bora, jamani watu igeni mfano sio kwakua mtu unakuwa celebrity basi unaachia hausgal ampikie mumeo na kumfulia hadi chupi, marufuku..
gud gal
mama brandon

Anonymous said...

heey gal...nimekubali....unapenda kupika!....mimi hata nifanyeje sipendi kupika kabisaaaaa....i used to think motivation ya kupika inakuja if ur man treats you really well...looks like Gardner treats you well and that makes you love him more and hence the motivation to cook....thatz my opinion...keep it up superwoman!!

Sab said...

Asante manka kwa Recipe ya Pilau.yani ndio mana Kaka angu Gadna ananenepa eeh mwanamke kupika mwenzangu mtu akikuona awezi amini unajua kupika ivyo.nakupa Big up dear.ur wife material

Anonymous said...

Manka naomba no yako au nifahamishe nitakupataje

Jide said...

Anony wa 1:25AM namba yangu ya simu iko hapo kwenye blog page ya mbele upande wa kulia kwenye contacts. ila kwa sasa kwakuwa niko safari, haipatikani. Unaweza kuniandikia email kama ni shida ya haraka sana. Karibu

Anonymous said...

Shida yangu ni Berna,email sina uwezekano mwingine

Anonymous said...

he jamaniii tumefungaaa wenzako ukooo


cute smile

Anonymous said...

Mrs Habash
tatizo lako hutaki kukosolewa unajipamba tu na comments nzuri nzuri humu za wasiojua kupika wenzio.
Pili namshukuru Anomy wa pili baada ya jacque kwa kutupa recipe ya pilau HALISIA na si Pilau yako VUMBI..huyo ndi mpishi haswaaaaaaa!!!!
Hata cku moja usirudie tena kupika Pilau la namna hiyo utaachwa tena una bahati sana mmeo wa bara.
Kama unanibania bana kama kawaida yako binti misifa lakini ujumbe received.

Anonymous said...

Wewe anony unayemwomba Mrs. G kwa ajili ya shida ya Berna kaa ukijua kuwa Berna ni mchumba wa mtu, labda kama unamtakia shida nyingine zaidi ya hiyo. Tafadhali angalia matoleo ya nyuma yaliyopita utalifahamu hilo. Ni mtarajiwa wa Venture kama sikosei.

Anonymous said...

Hiyo pilau ya kikwenu..duuu watu wa pwani wa kikuona watakushitaki lol

Anonymous said...

Manka ninachoomba unifahamishe kwa Berna sina nia Mbaya ni kumshukuru kwa kukupokea. Hata kama ni mtarajiwa hilo halidhuru.

Anonymous said...

wewe unayemwambia mwenzio kapika pilau vumbi, wewe lako la majivu likowapi? unamfagilia huyo alotoa recipe fake hapa, toka lini viungo vya pilau vikachemshwa?
kwa taarifa yako viungo vya pilau havichemshwi! unavisuuza/viosha na kuviroweka mapema tu (hata kwenye kikombe)kabla hujaanza kutayarisha vitu vyengine basi inatosha! na kama utatia karafuu basi moja au mbili tu inatosha ukitia karafuu nyingi na ukazichemsha hicho chakula utakula peke yako!
cha maana alichosema hapo ni kutumia supu, pilau ukipikia supu inakuwa tamu na ladha nzuri zaidi ya unapopikia maji.
Pilau hupikwa kwa kutumia viungo vizima na si unga. unga husababisha pilau kuwa nyeusi.
na mwisho najua mchele mmoja mapishi mbalimbali - Pilau hasswa haitiwi nyanya wala carrot.
Nawakilisha!

Sab said...

Nimjibu Anonymous 4:56 Unajua kila mtu ana mapishi yake so yeye pilau lake anapika ivi na wewe unapika vile tuletee na lako unapikaje.mana ata mimi pilau napika tofauti na Jide so usiseme ajui kupika na aliyekuambia mtu anaachwa kwa sababu ajui kupika pilau nani.Tuletee na wewe ufundi wako tujifunze kupika kama wewe mana umesema la Jide ni pilau Vumbi ha ha ha ha jamani watu hamna wema.Manka mama tuletee recipe zako tunakukubali Mrs G

Anonymous said...

Sorry sijatoa my receipe kwa ubaya Jide mwaya Sorry 4 this kama nimekuudhi ial nimesema kam kushare mapishi ila viungo unavichemsha kwanza ndo unatumia yale maji kama viungo jaribu uone aua nenda City Garden kale Pilau lao ndo utajua ni pilau la viungo vya kuchemsha mtt wa kike na ukitaka palilia waweka bizari nyembamba kwa chati linanoga upo wewe unaebisha ,Sijakupenda unataka ligi wakati tunaelemishana wanawake wakibongo kwa kupenda kudakia Usiuseemeee Moyo wa Jide

Anonymous said...

Manka mapishi huwa tofauti siku zote hivo waelewe wote na kukubali maoni.

Jide said...

Ni kweli mapishi hutofautiana ndio maana sijajibu lolote kwa wanaokosoa na kuleta recipe zao, kwakuwa huo ni mtazamo wa kila mtu bora mkono kinywani. Ila naomba mkiweza mnitumie na picha ndio itanoga zaidi

Anonymous said...

Manka najiweka vizuri nikutumie recipe usijali

Anonymous said...

Manka huyo anony anyemuulizia Berna huwezi kujua ana lengo gani maana sio wote wenye mawazo mabaya huwenda ikawa bahati yake.

Anonymous said...

hi, naomba kuwajibu anony wa 4:54 AM na anony wa 3:35 PM kwamba maana ya mchele mmoja mapishi tofauti ndo hiyo!! kwamba aliyepika pilau vumbi, pilau mchemcho sijui pilau bokoboko zote ni pilau na zimetumia mchele mmoja na zina ladha tofauti kila moja, na ukionja moja utajuta kuifahamu nyingine!! viungo vya pilau (baadhi ya pishi) vinachemshwa me mwenyewe nimeshawahi kupika nakula pia, try to test it an'u will see. So, kama we unajua aina moja ya mapishi usimkosoe mwenzio anayejua aina tofauti, jaribu kupika na uonje ladha yake!
swaumu njema!!

shushu 'hot'

Anonymous said...

unayesema unayatumia yale maji kupikia una maana viungo unavitupa au? tueleweshe.
maana nijuavyo bila viungo vizima ndani hilo si pilau.
city garden nini?! ingia majikoni kwa wenyewe uone!
unataka kuniambia biriani ya mahoteli ndio biriyani?!
toka lini muhamadi na wanja?!

Nkyekuu said...

Nashukuru kwa recipe ya pilau la kuku,hilo pishi la tambi za maini nalisubiri kwa hamu manake yaani kulitamka tu tambi za maini mate yananijaa mdomoni.enjoy u'r holiday!!!

Anonymous said...

i like u the way u are my sis,keep it up,na unapendeza ana nw days my sis.napenda mapishi unanikuna kweli na blog yako shost the way unavyojibu comments za watu,i really apprec8 u.thanx stay safe

alexandra said...

asante dada nimelielewa pishi lako naenda kulipika alafu nita kupa matokeo.uko juu na kukubali sana.endelea kutupa vi2ziii!

Anonymous said...

jaydee na wadau wa blog hii, nisaidieni jinsi ya kutengeneza chicken sekela, jamani napenda aina hii ya kuku hasa ukila na viepe tamu mno, ila sijui inatengenezwa vipi,msaaada plz

mrs don

Anonymous said...

Jaman mchele mmoja mapishi mbalimbali

Roller skate in TANZANIA said...

mbona recepe zinazotakiwa hauziweki yaan vile viungo
halafu upost in english coz nipo nje yanchi and maduka ya huku kuna viungo vengine hawavijui niwatajia kiswahili