Wednesday, October 7, 2009

RECIPE YA WIKI HII...CHAPATI ZA KUSUKUMA...Naombeni msaada kwa anaejua jinsi ya kuzipika, Mimi nikifanza hazitoki za ukurasa, zinakuwa ngumu kama ngoz


49 comments:

Anonymous said...

Hata mimi naombeni nifundishe kupika chapati natanguliza shukrani

Anonymous said...

Jide naona unashangaa comments zangu za mwanzo ni mie niliesahaulika naifanyia kazi ahadi yetu

Anonymous said...

jamani jide kwanini tusipike chapati za nyama za kusaga.mwezangu chapati hua hazinaga siku siku zinatoka nzuri siku nyingine mswalie mtume kitu kinatoka ngozii yaaangu ngumu kama upo karibu ya ukuta unaweza ukaona nyotaaaaaa.

cute smile

Anonymous said...

Jide fanya mpango tuwe tunachat humu

Maryam Yahya said...

Mama..hata mimi zilikua zinatoka ngumu kama mkate wa bati,kumbe ni swala dogo 2.ukiwa unakanda tumia warm water with salt na mafuta kidogo usiweke mafuta mengi.kanda mpaka ilainike .Then ukiwa unakunja isukume sana na ipake mafuta ya kutosha kisha ufunike mpaka time ya kuchoma usiziache wazi.

*pia kuna mtalaam mmoja wa chapati magomeni alinitonya kua hua anachanganya unga na maziwa ya unga kiasi(NIDO)..chapati zake ni tamu ajabu.

Mwanamke mapishi.

Anonymous said...

haya Recipe ya chapati kutoka kwa Mumy G,Swiss, Gnv
1 chukua ngano yako weka kwenye sinia kavu
2,weka chumvi ya unga,changanya unga
3, chemsha mafuta yako yoyote yakishachemka, yamwage kwenye unga wako changanya na mwiko ukiona umechanganyika yani kupoa kwa mafuta changanya sasa na mikono
4, weka maji ya uvunguvungu changanya unga, hakikisha unakuwa laini, usiwemgumu kama wa halfcake,
5, kata matonge matonge, ukimaliza kukata matonge
6, sukuma hata kama isipokaa vizuri ni ipakae mafuta,ikunje fanya hivyo katika matonge yote uliyokata,
7, pandika chuma chako cha kuchomea chapati, sukuma tonge la chapati hakikisha sasa ukisukuma inakuwa duara,halafu weka kwenye chuma chako kilichopata moto wa kiasi ukishaona upande umeiva geuza mwengine halafu weka juu yake chapati nyingine fanya hivyo hivyo kungeuza kila upande ,pande zote nne zikishaiza weka mafuta ukigeuzageuza kila upande, hapo utakuwa umepika chapati mbili kwa mara moja fanya hivyo kwa zote kwa kupika mbilimbili
8, hakikisha unazifunika kila ukizitoa jikoni

Anonymous said...

waswahili bwana..Mtu anauliza asaidiwe kupika chapati..watu mnaandika mambo mengine..kazi kwelikweli

Christine said...

Manka mi nilijua hilo tatizo la kwangu peke yangu, hata mimi nikipikaga zinatoka mfano wa gome la mti. Ukiing'ata hadi meno yanauma.

Anonymous said...

mie ndio sijui ht kidogokuhusu upishi wa chapati za kusukuma,mnyonge wangu ni zile za maji.wataalamu tupeni somo

Anonymous said...

Hakuomba asaidiwe kupika,ni jinsi ya kuzipika mi najaribisha nitakupa jibu, ahadi ipo bado.

Anonymous said...

Jide asante humu tunafundisha mengi

Anonymous said...

Jide lini utaweka chat tujibishane humu

Chicken Finger Lickin ..Cluck CLuck said...

na mimi nataka kuwafundisha kutengeneza chiken finger lickin..mko tayari?

Jide said...

Asanteni Maryam Yahya na Mumy G, wa GNV, Swiss. Hili zoezi nitalifanya jumamosi kwakuwa ndio sina Sanya Sanya halafu nitawapa majibu kama nilifanikiwa ama la. Wale wanaojua kupika maandazi ya nazi andaeni recipe wiki ijayo ni hayo na chai ya tangawizi. Asanteni sana wapendwa wangu wote, zikitoka vilivyo nitawatafutia zawadi Maryam na Mumy G.

Anonymous said...

Jide upendeleo ni kwavile wamekupa recipe na mi nilietoa ahadi naifanyia kazi huna mpango nami

pam said...

mmh hata mi mwaya niliwahi pika chapati almanusura watu wang'oe meno yaani asubuhi ilipofika ndo ukikata yalia kakakakaka....ndo nikaelekezwa nitumie maji moto so hapo naanza kukanda na mwiko nikiona umoto umezidi...nihakikishe umelainika kabisa...na kuna mwingine alinambia nikitaka matokeo mazuri zaidi mafuta ya mgando kama kimbo etc ni best kwenye kukandia chapati...hapo hata kama ni siku 2 zitadunda bado laini...

Anonymous said...

Kanda unga na maji ya moto...

Jide said...

Mdau wa Dr. Dre we nifikishe kwanza hollywood halafu uone mambo. Swala lenu la kuanzisha sehemu ya ku chat nalifanyia kazi nipeni muda nimtafute DJ Choka mtaalamu wa majamboz anirekebishie chat room

Christine said...

manka na mimi ntaenda kujaribu tumenufaika wote kupitia wewe, mmh thanx

Anonymous said...

Jide nitakufikisha ndio nalifanyia kazi subira yavuta heri,Hiyo chat itakuwa ya nguvu.

Mama Nyanketa said...

well hi guys im new on this blog came across this article haya if u want the best chapatti ever this is my family recipe huwa haturuhusiwi kuzitoa isipokuwa nimejifunza uchoyo wa maarifa sio mzuri thats why nimeamua ku share na nyie wenzangu.

chukua unga kilo moja ambayo utatoa chapati 10 au 12 tu usizidishe,yai moja,Nazi kopo moja na butter stick moja tu ukikosa ya moja moja unaweza kuchukua moja kubwa ikate mara nne.na chumvi kidogo changanya kila kitu pamoja kanda unga.
halafu kata madonge wakati unazikunja changanya mafuta na samli na siagi kunjia then after that sukuma uchome ukishachoma unatia samli kijiko kimoja kikubwa usitie tena samli ukiigeuza.

ukifatisha hii recipe kila mtu atakuuliza umepikaje na unaweza uka kaa nazo hata siku nne ukiipasha moto kwenye mcrowave 1 min au hata kwenye jiko inarudi kuwa laini kama kawaida utasema umeipika leo....try this and tell me the reults....enjoy ur chapatis..and luv u all

Anonymous said...

Kandia maji ya moto ila yasiwe ya moto sana. Ukishakanda unga wako uweke ktk mfuko wa plastiki na uufunge huo mfuko na subiri dk 10-15. Anza kukata madonge na sukuma halafu paka mafuta na kuviringisha halafu weka ktk beseni na ufunikie kila unapomaliza kupaka mafuta.Wakati wa kusukuma madonge ulioisha kupaka mafuta uanze na donge la mwanzo ulilolianza kupaka mafuta. Hii inasaidia uingiaji wa mafuta.Na kisha choma chapati zako. Kumbuka usiziunguze.
Tumieni cowboy kwaajili ya kupaka na kuchomea tumieni mafuta ya maji.
Atakaeshindwa kabisa au mvivu wa kupika aende K,nyama opposite na shule ya msingi k,nyama nje kuna makaburi na kuna geti la bati na kiduka kidogo. kuna wamama wanapika chapati ni balaa nenda katoe order au ongea nao wakufundishe kwa vitendo. Gharama za kujifunza sizijui.

Anonymous said...

tumia maji ya uvuguvugu na mafuta moto ( mia huwa nafanya hivyo) ukiamua tia na mayai au maziwa pia mazuri kanda kwa muda hadi unga ulainike.

helen

Anonymous said...

Mama NYANKETA what is butter stick?
na kama hauna samli unaweza kutumia siagi tu? nimeipenda recipe yako I want to try it

mama Nyanketa, Maryland said...

butter stick ni siagi ile imekaa kama donge kubwa moja yaani cube kama kipande cha mbao huku kwetu zipo ambazo wamezigawa tayari in 4 pieces kama sticks hivi sasa ukikosa ambazo tayari zimekatwa unaweza kuikata mara nne yaani kwa urefu wa vipande vya mbao. its a good recipe jaribu utaipenda n u will be the best kwenye upishi wa chapati yeah kama hauna samli unaweza kutumia siagi na zinatoka nzuri tu ila ukijitahidi kupata recipe niliyokutajia utatoa the best chapatis ever.

PM said...

Kaazi kweli kweli leo humu, Marehemu Mom wangu used to fry the best chapo i have ever had, sorry she is no more, ningemuuliza, maana namind chapo vibaya na nasikitika hata Jide anapika kau kau badala ya chapo, hope kuanzia kesho kwa maelezo ya wadau mbali mbali mambo yatakua powaaaa!

Anonymous said...

Mama Nyanketa cheers!!

Anonymous said...

Mama Nyangeta naomba unieleweshe hiyo butter stick ndio nini?

Anonymous said...

Mmh! Kweli mchele mmoja mapishi 100. Naona tu huku nazi, butter stick,yai sijui. Fat juu ya fat! Chapati imekua cake andazi Teh eeh ee. Me yangu simple tu na inatoka wow! Weka unga wako kwenye chombo unachotaka kukandia, kilo moja ya chapati yatoa chapati 8 hadi 12 inategemea na size unayopenda. Weka chumvi kidogo,mafuta ya kupikia(ya baridi)kidogo ama vijiko 2 vya samli. kisha chukua maji ya baridi hata km yametoka kwenye fridge yafaa. kanda taratibu, usiwe mgumu sana wala laini sana. Ngano ikiwa tayari utaona tu inazidi kulainika jinsi unavyoendelea kukanda. Unaweza ukasukuma moja kwa moja, ama ukitaka ziwe laini zaidi funika unga atleast one hr. Halafu utatengeneza duara ndogo ndogo kutokana na size uipendayo! Sukuma mduara paka mafuta ya kupikia kidogo ama samli km unapenda kisha ikunje. Endelea kufanya hivyo mpaka unamaliza miduara yote then utaanza kusukuma tena na kuweka kwenye kikaango tayari kwa kuchoma. Hakikisha chuma kimepata moto b4 kuchoma. Usiweke mafuta, ichome chapata pande zote mbili ikishabadilika rangi kuwa brown ndo paka mafuta upande wa juu kisha igeuze, fanya ivyo na upande mwingine igeuze mara mbili tatu kisha itoe. Endelea kwa mtindo huo mpaka utakapomaliza chapati zote! Nafikiri umenipata. Cheers!

JO said...

Kumbe chapat za kusukuma ugonjwa wa weng sio mie tu asante mliotoa recipe na mie napumzka za kumimina mwendo kusukuma

Anonymous said...

Sasa Jide huna kisingizio cha kushindwa kumpikia chapati Cpt, Shule ndio hiyo mpaka mlangoni nini tenaa,

Utasema mkaa umelowa au luku imeisha na ile foleni ya majuzi imerudi tena???? hahaaahaaahhhhh!!!

Asia said...

Hi jide, ili chapati ziwe laini anza kuweka mafuta ya kupikia ya moto kwenye unga na kandia maziwa au maji ya uvuguvugu na ukishakanda cover vizuri ili hewa isiingie.

ck said...

Thanks Jide kwa mawazo yako, coz inatusaidia hata sisi tusiojua kupika chapati, Jumamosi nitajaribu. thankx mumy

Dorry said...

Nipeipenda recipe ya mama Nyanketa. Be blessed. Thanx to Jide wote tumeelimika.

Frida said...

asante sana jide hata mimi nimejifunza mengi. ila kila mtu ana ujuzi wake unaweza usiweke hata samli na bado zikawa yellow pages(yani vidole vyako vinatembea)
mimi uwa natumia maji na mafuta ya moto tu nazina toka bomba ila kukanada ndio mapishi yote na wala sio kuchoma ukikanda vizuri basi hapo umemaliza kila kitu.kuhusu maji maji ya uvuguvugu ni mazuri zaidi. ukishindwa nialike siku moja nije nikuonyeshe mapishi ya cahapi za ukweli.

frida said...

asante sana jide hata mimi nimejifunza mengi. ila kila mtu ana ujuzi wake unaweza usiweke hata samli na bado zikawa yellow pages(yani vidole vyako vinatembea)
mimi uwa natumia maji na mafuta ya moto tu nazina toka bomba ila kukanada ndio mapishi yote na wala sio kuchoma ukikanda vizuri basi hapo umemaliza kila kitu.kuhusu maji, maji ya uvuguvugu ni mazuri zaidi. ukishindwa nialike siku moja nije nikuonyeshe mapishi ya cahapi za ukweli.

Mswazi said...

mk kumbe maziwa yalainisha chapati.But how comes,walimu hapa mmenichanganya kabsaaa.

Anonymous said...

Anony October 7, 2009 11:25 AM....u didnt have to critisize by saying fat juu ya fat ulitakiwa utoe tu recipe yako mama Nyanketa amejitahidi kutupa ya kwake. na wengi wetu tumeipenda hizo chapati zenyewe zako unazotia samli pia ni fat..kuwa mstaarabu amepoteza muda wake to share with us her family recipe wewe maneno yamekutoka lakini kama ulivyosema mchele mmoja mapishi 100 big up mama Nyanketa n im sure Jide pia ameipenda recipe ya mama Nyanketa.

lady dath said...

mm kwa nnavyojua uuwe na unga blue band au mafuta kawaida,maji,nazi au maziwa iriki sukari kidogo na chumvi kwa wanaopenda,then unapasha mafuta yako unaweka pembeni na maziwa ukiwa umechanganya na viungo then utachanganya unga na chumvi mpaka vicanganyike,then utaweka mafuta huku ukichanganya na maziwa mpaka unga uwe mzuri jinc unavyopenda mlaini,utakata maduara maduara kwa njinci ya idadi unayotaka then utaanza kuzisukuma ili ukunje make sure unazinkunja kwa kutumia mafuta,ukishamaliza utasukuma na kuzikaanga usipunje mafuta cz yanasaidia kuzilainisha kwa nnavyojua mimi cz kila mtu ana utalaamu wake,thanx cicy manka am new kny blogger yako hope utanikalibisha vizuri ili niwe fan wako much luv ya.

Anonymous said...

shukrani kwa kuleta hii kitchen party ya chapati manake mh ilikuwa ni aibu zangu zilikuwa ngumuuu hadi meno yanachoka kutafuna asante mama nyanketa recipe yako nimeikubali hii nitaiandika kabisa hadi kieleweke
mdau canada

Anonymous said...

Kwa kweli Jide umetusaidia wengi, na tunawashukuru wote waliotoa recipe zao, upande wangu mie ntajaribu nyingi kadiri niwezavyo!

Manake ilikuwa aibu, niliwahi kupika zangu halafu tukawa na mgeni. Mgeni anakata chapati inakatika kwa mlio..kwachaaaa...karibu niingie chini ya meza kwa aibu! mpaka leo najiuliza ni kiherehere kipi kilichofikisha chapati zile mezani! lol!

Anonymous said...

yaani mpenzi Jide hiyo RECIPE ya chapati niliyokupa Mummy G, wa Swiss, Gnv wewe jaribu tu halafu utaona matokeo yake naukipika ujiamini kuwa leo wapika chapati ikiwezekana vaa kaghaa moja tu, nakuapia chapati itachambuka kama fedha, halafu uandae na samaki wa kupaka na chai ya maziwa ambayo hujachanganya maji hata tone na juice ya kutengeneza wewe mwenyewe na brenda yako ya matunda yoyote mumeo ayapendayo,jamani wapendwa msije nambia natoa kitchen party no, ni chapati tu

Anonymous said...

yaani mie kwa chapati kwa kweli zinatoka laini kweli na tamu kweli kila nikipika mtu hushindwa kutosifia chapati alokula kwangu,nachapati mie huku niliko hupika nakula hata mie mitatu naweka kwenye friza,ila huwa nazipanga kwa mafungu ya idadi nikizitoa kwenye friza basi hizo zitaliwa zote

LaMbegu said...

Mama nyanketa hiyo recipe yako utauawatu. Huitaji mayai na siagi. Dawa ni kuhakikisha kuwa unga nilaini kabla ya kuanza kusukuma. Maji ya vugu vugu na chumvi ni tosha.

mama Nyanketa, Maryland said...

hahahhahh LaMbegu.....sio mayai its 1 yai na siagi sio lazima iwe yenye a lot of fat unaweza kutumia light version n also sijakulazimisha utumie recipe yangu unaweza kutumia yoyote inayokupendeza na also hukuambiwa ucritisize umeambiwa utoe recipe yako thats how i cook my chapatis n my husband likes them na kila anayekula my chapatis anazipenda na kuniuliza how did i cook them.....upo hapo LAMBEGU? kama unavyojua mchele mmoja mapishi tele tele.do urs and ill do mine n whoever want to use my recipe gudluck sijakulazimisha.Have a nice day LAMBEGU

Ommy said...

Thanks Jide and your fellowers,it was great to visit ur blog,I manage to make Chapatiz,my freinds was very happy.Great Job! Ommy, Cape Town

Anonymous said...

well,me and my baby tried.we failed miserably.Maybe next time.

Anonymous said...

Siri ya chapati kuwa laini ni maji kuwa ya uvuguvugu mkali na kusukuma unga kuwa laini yaani lile donge lisiwe gumu likiwa gumu ndio ukavu wa chapati.

Anonymous said...

Mmmmmhhh