Friday, February 5, 2010

ALAMA ZA WAABUDU SHETANI.???????.......IMETUMWA NA FRIDA LUKINDO

Mchungaji Joseph akiwa stendi ya Ubungo

Kuna mtumishi kutoka Kenya yuko Dar es salaam anajulikana kama Mchungaji Joseph, amekuwa akizunguka vituo mbalimbali vya daladala akihubiri habari za Mungu na kusema mambo mbalimbali anayoyaita ni siri za shetani na kazi anazozifanya, Pia ni kwa jinsi gani watu wanachukuliwa misukule!
Mtumishi huyu alielezea aina ya nguo ambazo zimetengenezwa kuzimu na Mtu akivaa hizi zenye wanyama hawa, huonekana moja kwa moja kwenye ramani ya kuzimu
Alielezea kwamba aina ya nguo hizi mtu akivaa haishi miaka mingi, au kufa kifo kisicho cha kawaida

Pia alielezea huyo mnyama yupo anaishi baharini hivyo hiyo siyo picha tu!

Pia kulikua kuna kitambaa ambacho kilikua na alama mbalimbali ambazo anasema wanatumia wanaoabudu shetani au Freemasons. Na kusema pia wapo watu wanaosema ni wakristo wanatumia baadhi ya hizi alama hizi kwa kujua au kutokujua!

Pia lisema kuna wahubiri wawili ambao wanahubiri kwenye TV wanahubiri na kuponya kwa nguvu za giza ambapo wanatumia PETE zenye nguvu za giza . Ameliasa kanisa kuombea kazi ya Mungu kwa kumaanisha maana wapo watu wamejiingiza kanisani kama kondoo kumbe ni mbwa mwitu.
Alipokua akihitimisha mahubiri yake, alitaka watu watoe mafungu yao ya kumi na sadaka, pia aliwaombea wote waliokua na mahitaji mbalimbali.

14 comments:

Anonymous said...

mie niko hapa sweden kuna siku nilimuuliz mtu unajua kuhusu freemason akaniambia ndio hata hapa sweden wapo,akasema twende nikupeleke lilipo jumba lao,basi tukaenda hapo lkn huwezi kuingia zaidi ya ktk kibaraza chenye ngazi.yaani ni pazuriii hizo ngazi ni nzuri halafu kuna mialama alama kama hiyo ktk hicho kitambaa halafu kuna weird hisia nilipata yaani nywele zilisisimuka halafu kumetuliaa na roho yangu ilikua inadunda sana basi nikasema kwa kiswahiliDAMU YA YESU TENDA KAZI YAKO HAPA kisha tukatoka tukaendelea na mizunguko mjini,sasa cha ajabu kila tulipoenda kuna kijana alikua nakutana naye mwishowe nikagundua alikua ananifuatilia lkn alikua anajifanya ana hamsini zake nikaogopa kishenzi sasa kuna mahali nilikua natoa hela ktk ATM kugeuka nyuma na yeye yupo basi nikaanza kusali nikasema SHETANI USHINDWE KTK JINA LA YESU nikashangaa akaondoka kabla ya kuchukua hela halafu nilivyochukua baadae tena nikawa nakula sousage mahali mara ikatokea limousin yenye wazee wengi ndani ikawa inapita taratibu huku watu garini wakinitizama nikamuona na yule kijana yumo.

Anonymous said...

Washindwe tena waregeeeeeeeeeee
EE MUNGU TUEPUSHE NA HAWA IBILISI WATU WANAOTULETEA MAJANGA KATIKA NCHI YETU NA DUNIA KWA UJUMLA.

disminder

mama Nyanketa, Maryland said...

Well Nataka tu kuwapa ufahamu wangu kuhusu hii Freemason.sio waabudu shetani ni chama cha watu wenye mtazamo wao kuhusu dini kwani ni chama kisichohusiana na kujishirikisha na dini yoyote infact kila mtu anaruhusiwa kujiunga na sio tu kujiunga unaweza ukajiunga kiholela hapana inabidi upitie matabaka maalum amabapo inabidi mwanachama aliyeko ndani pia aku recommend kusema ukweli ni chama cha watu wakubwa na waziti kwenye nyadhifa mbalimbalia na ukibahatika kuingia kwenye chama hiki utakuwa unasaidiwa sana na ku boostiwa mambo mengi sana hiki chama wanasaidiana sana kwenye maendeleo na hadi kesi hata kama una kesi kubwa kiasi gani ukiwa mahakamani ukitoa ishara ya kuwa wewe mason na jaji kama ni mason anakuacha u slide kesi inafutwa bila hata kujua na huku mamtoni ukikamatwa na polisi kama ni mason na yeye mnapena ishara zenu za kutambulishana anakuachia.kama una biashara yako ukiwajulisha wanachama wenzako wanakupa tafu ile mbaya. mimi binafsi nimesoma kuhuu hiki chama na nimeona kuwa sio chama cha kuabudu shetani ni kama vile unapokuwa na organization fulani halafu una muswada wa hiyo organization yako na unakuwa na miundo mbinu yako na mikingamo yako katika chama hicho. kusema ukweli ni ngumu sana mpaka kujiunga na chama hichi ndio maana walioshindwa kukubaliwa kujiunga ndio wameamua kutangaza kuwa ni cham cha wanaoabudu shetani lakini la sio kweli ni chama cha kusaidiana lakini wenyewe kwa wenyewe wanachama. na nitaendelea kusoma more about it then will keep u posted so that u understand what its all about.

ngaizaskids said...

Ee Mungu utusaidie, kweli hiyo alama inatumiwa na wakristo wasiojua kama ni dhambi, manake utakuta watu kibao wamevaa viatu, t-shirt zenye arama hiyo.

Hata mi naishi uswid ila sijapata kufika sehemu yao hao watu, iladarasani kwetu wapo kibao, wengine unakuta wametipaka rangi nyekundu na nyeusi kichwani, nguo nyeusi na nyekundu na viatu hivyo hivyo, alafu wanavaa kila siku. Washindwe kwa jina la Yesu. Mungu ni mwema.

Anonymous said...

....hana lolote huyo kwanza yeye ndio mwabudu shetani.we toka lini mungu akaua watu kwa vifo vya ajabuajabu?hiyo si ndo kazi ya shetani....?!
nachukizwa sana na watu hawa kujifanya ndo wamemwona mungu kumbe wanachotaka ni kuwanyonya watu tu ambao wanachukua muda kuwashitukia.kila siku siku hizi kuna mtu anajiita nabii,muhubiri na mengine mengi,hawa ndo waabudu shetani wenyewe.kwani huko kenya alipotoka ameshindwa kupata watu wa kuwahubiria mpaka aje tanzania...?!
kwa kweli inabidi tuamke kwani haya makanisa kila siku na wahubiri wa uongo hawalao kubwa ni kupata watu wawalaghai kisha baadae haoo wanaingia mitini.
mi nadhani kikubwa ni kuwa na imani yako tu.mpende jirani yako bila kufanya maovu ndio kitu cha msingi na sio kuwasikliza hawa walaghai wasiokuwa na mbele wala nyuma.kazi yao kunyooshea vidole wenzano na kuwaona kuwa watenda dhambi wakati yao wanayasahu matokeo yake ni kuwafanya watu kubaguana kwa kuwa wanaona wengine ni watenda dhambi.nani kakupa wewe mamlaka ya kuhukumu na kunyooshea kidole wengine...?!.
achana na utapeli huu....

Anonymous said...

Pole sana Anony you realy have to nill down and pray so that they get out of your life, they will haunt you untill they know where you stay and probably do some thing terrible. Nill down every day and talk to God and cover your self with the blood of Jesus christ, but you havent told us what happened in the end....... mh please finish the storry it was kind of intresting.

Anna

Anonymous said...

Mwe jameni mie mneniacha hoi!.. kama shetani ashindwe,
lakini makanisa haya, wengi wanataka tu hela na anajua akishakutia woga, basi utatoa hadi mafungu arobaini ya sadaka.

Halafu hiyo picha ya pili, mbona ni kama Chinese Dragon. Hapa USA wachina wanasherekeaga Chinese New Year na wana madragon kibao, kwao ni kama hadithi za kizamani vile.. au na wenyewe ndo mashetani tena!?
tuelimishane basi, na mtu utumie facts sio maneno tu...
au sio?

Anonymous said...

mbona hata hapa bongo hilo jumba lipo pale mtaa wa sokoine walikua wanaliita lodge au temple na kuna siku nilienda jumbani kwa judge mmoja nikafika nikakuta vitabu vingi kwenye coffee table vinahusiana na hiyo freemasons ndipo niliposoma kanisa lao lilipo. Nikaogopa judge alipokuja sebuleni akavifunga na kuviweka ndani nikamuuliza rafiki yangu kwamba vile vitabu ulishawahi kuvisoma akasema hajawahi na yeye hayuko interested sana na kusoma soma vitabu ila mdogo wake aliuliza akajibiwa ni vya lions na rotary club ni google hao freemasons nikaona kwamba wanauhusiano sana na hivi vyama vya misaada ya kibinadam esp. watoto.

sophia said...

jamani mwisho wa dunia unakaribia neno la mungu ni kitegauchumi makubwaa!

Anonymous said...

Freemason ni dini ya kishetani, wewe acha kuwadanganya watu eti ni chama cha kidini, mwenye masikio na asikie, jide kafanya kazi ya Mungu kuwatahadharisha. Wewe unaeamini hao freemason, kaa na imani yako usipotoshe wengine.

Anonymous said...

Freemason sio chama cha kidini ni social club sema ni the powerful one kwa ajili ya watu wa kubwa na wenye nyadhifa kubwa kubwa katika kila pembe ya dunia. na sio dini ya waabudu shetani.

Anonymous said...

KUHUSU NIKE HAPO MMEONA NIKE MAANAYAKE MUNGU MWANAMKE UGIRIKI NA KAPA NI WANAZINI WAWILI WA KITALIANO. HIYO NILIONA MIAKA MITANO NYUMA KUNAMTU WA DINI YA KISLAMU ALINIAMBIA NIKAMKATALIA.

Anonymous said...

wanasema ukiweza kudhibiti historia umeweza kudhibiti yajayo,hawa watu wapo toka zamani za miaka ya 1600,wako katika kila sekta kny maisha ya mwanadamu,ni vizuri kujua historia kisha kuoanisha matukio na hata kuoanisha maandiko ya MUNGU yanasemaje kuhusu shetani na wakala zake,wanakuambia wao ni wanajamii wa kawaida lakini unaijua historia yao?wanatumia alama na ishara kadha wa kadha na kutolea fafanuzi wajuazo wao nawe wakubali ni kile wasemacho,hakuna mtenda maovu akasema ni mtenda maovu.mtu anaweza kupambana na mazingira yake kama anakua na maarifa nayo,pateni maarifa toka ktk tovuti,wavuti nk. mtu awezejua freemason ni watu wema au wakala wa shetani?mambo yote yako wazi,na MUNGU kamwe haachi siri bila kuifichua,ilikua ni siri wakiitwa secret societies ila siku hizi si siri tena mambo yote hadharani

Anonymous said...

Huyo anaesema frmsr ni chama cha misaada ya kijamii tu anaijua? Au na ye ndo muumini? Usitake kutetea kitu usichokijua, uliza ex-members wakujuze yaliyomo kwenye mason