Wednesday, February 17, 2010

NYOTA NDOGO AKANUSHA MADAI YA GAZETI LA RISASI

Tofauti na habari ilioandikwa na gazeti hilo kuwa alijivinjari na mchumba wa mtu siku ya Valentine alipokuja kufanya show yake hapa jijini Dar es salaam.
Nyota amesema kuwa huyo ni bouncer aliekuwa amepewa kuwaangalia na kuwasaidia.
Na kuwa hata aletwe hapa leo hataweza kumkumbuka sura yake.
Hapo alikuwa anapewa msaada ili aweze kupanda jukwaani na si vinginevyo.
Nyota Ndogo anawaomba washabiki wa muziki wake hapa Tanzania na kwingine kote habari hiyo ilipoenea, kutoamini madai hayo yalio andikwa na gazeti kwa kuyakanusha vibaya sana.

Na anategemea kuondoka siku ya Alhamisi kurudi nyumbani kwao Mombasa, ila kwa sasa bado yupo Tanzania akimalizia kazi mbali mbali zilizomleta


7 comments:

chib said...

Wabongo mie ningewasifia sana kama wangekuwa wanaandika habari za ukweli na kuleta maendeleo, ikiwa ni pamoja na kuwanyanyua wasanii. Hata kama gazeti ni la udaku, basi liandike habari ambazo zina ukweli na zilizochunguzwa. Sio kwa nia ya kuuza gazeti kwa kuandika habari ambazo hazina mikono wala nywele!

Anonymous said...

Hata Picha inaonesha Kama si ya kiuchumba ni mapendo tu ya Bouncer ya Msaada jamani haya Magazeti kazi yao kuharibia watu tu.

Mtu akiumwa wanaandika anaumwa Gonjwa moja baya sana ili watu wafikirie na ukimwi kama walivyomuandikia Mzee ngurumo Mkuu wa Msondo Ngoma Maskini anamatatizo ya Miguu mungu amsaidie apate uzima.


Au Dada Yetu lady jay dee mtu ukiumwa unapendwa zaidi na mungu kama walikuwa hawajui. Seif.

shostito said...

mhh magazeti yetu nayo!mhh sometimes yanazidisha.pole dada lkn hiyo picha nyingine mmmmh!! bouncer huo mkono ulikua unafanya nini begani au ndo alikua anakuzuia usifatwe na watu! mh haya ukweli waujua mwenyewe

sophia said...

Hivi haya magaze4ti ya udaku hayafungiwi yote kwanini? maana kila siku huandika habari za uzushi na uongo tu , serikali iwafatilie hawa watu na wawekwe ndani ndio watakoma umbea wao!

Anonymous said...

Tunaonyesha nini kwa wageni kuandika habari za uongo?


disminder.

Ester Ulaya said...

Ujue asilimia kubwa ya sisi binadamu huwa tunapenda ku Conclude kitu kabla hatujahakikishiwa jambo, hao wa magazeti ni binadamu, nadhani ilitakiwa wawe na uhakika na waambiwe na muhusika mwenyewe kuwa huyo ni mpenzi wake, ndio maana inakuwa inaleta mitafaruku sana katika jamii.

Pia Human rights hapa kwetu Tz haizingatiwi kabisa, watu wanaona raha kupublish issue za mtu popote tu bila ridhaa yake, je ingekuwa huyo aliepiga hizo picha awe ndio yeye angejisikiaje?

Tutafakari jamani, tusizingatie biashara tu na kuuza bidhaa, kwanza utu wa mtu maswala mengine baadae

Ni hilo tu, pole Nyota

Anonymous said...

Atakuwa nyota kubwa sasa hivi huyu nyota ndogo!