Wednesday, June 30, 2010

MAISHA UPANDE WA PILI WA SARAFU 1.

Wakatiwengine wanavaa viatu vya kuanzia laki moja kwenda juu wengine wanatembea peku mpaka miguu inaota magwambala

Wakati wengine wanatumia majiko ya gas na umeme wengine wanatumia majiko ya aina hii.
Hili linasifika kwa kubania matumizi ya mkaa

Wakati wengine wanaendesha Lexus, Vogue, Hammer nakadhalika wengine usarifi wao ni baiskeli... Wanasema hata ujenge hekalu lakini chumba utakacholalia ni kimoja tu
Pesa haina maana yoyote sometimes, ukipata toa na tumia.


Wakati wengine wanakula kuku wa kwenye mifuko wa supermarket wengine wanafuga wanachinja wanakula.

Ila hii nimeipenda sio shida manake watamu hawa


Japokuwa hii ni blog ya Party, Burudani na Starehe lakini tuangalie na Upande mwingine wa maisha ya wenzetu


Picha zote za matukio: Na Esther Ulaya

13 comments:

Baby Anna said...

duh hiyo miguu jamani dah!
inanikumbusha mbali mie jamani
any way yote maisha lakin!!!

Anonymous said...

Ila usafiri wa baiskeli ni mzuri.Huku Holland ndio usafiri wa raia japokuwa si maskini.

Badi said...

Big-up Esther
picha ni nzuri kweli umejaribu kuonyesha hali halisi ya maisha ya wapiga kura... Are you a photojournalist? Nataka nikupe ofa..

Anonymous said...

me naona sisi ambao hatuna maisha hayo kwa sasa ni kumshukuru mungu. na tusisahu kuwa huko ndo tulipotoka, hata baba ako akiwa nani chimbuko lake ni huko tanzania hii hakuna mtu aliyezaliwa anazo, wote our source ni fresh form bushi.tena starting with 0

me nakumbuka kwani nimetokea huko kuni hizo nimetumia saana, na nimeokota . tena umbali wa masaa ma2 ukondoka saa kumi na moja unarudi saa 2 au tatu, mbali jide wewe milima usiseme ila huko ukienda kuna matunda, kuna kuni unakuta zilisha kaukaga we unavuja, tu unachukua mti ambao mbichi, kuna miti fulani inaitwa mikwee unachuna kamba unapanga kamba chini unaanza kupanga kuni. mpaka unakuwa mzigo, unafunga vizuri unaweka kanga unazungusha unaitwika kichwani unaleka kuni juu. nyuma umebeba kama mtoto matunda, mnatembea mkifika sehemu natua mnaanza kucheza mdako, wenye kula matunda, kama ndo ulipika kamkate au viazi unakula,na maji safari inaanza, mbali huko, we jide maisha haya ni kumfurahia mno mungu. na kumtukuza vipasavyo, leo hii mtu unamiliki kila kitu cha thamani kazi nzuri maisha mazuri, kweli binadamu unapitia mengi. ila tu be honest maisha hayo nimepitia,

ila sijawahi kwenda gesti, pia mchuchu wnagu alikuwa handsome jamani wee msafi sana, basi akija anapiga mluzi, unajua amepita unaenda kwenye geto lake, poa, sijui aliendaga wapi, naye long about 30 yeaers,

hapo umefua kakanga kako vizuri ndala sky way, unazijua wewe au viatu roso, umefua vizuri kanga umeweka bluu, umejifunga lubega maana miaka yetu tulikuwa tunajifunga lubega kuhofia kuonekana matiti. basi hapo umepaka shanti, snow, nywele umelambisha, umechukua kibati toboa toboa then kwenye moto halfu unalambisha sister du si wewe, nani atakugusa. sasa kama wale maadili kidogo kwao pungufu walikuwa wanajifunga kichwani kanga style inaitwa usongo wa pochi, maza angu akikukuta umejifunga hiyo hutoki na anapewa kazi ya kupukuchamahindi hata fuko zima.

maisha jamani ni safari, ndo manaana msemo wa mpoto ukiwa upo unasafiri miti inarudinyuma ni mweli unapiata milima, kila kitu ile ishara kuwa unatafua unakokwenda unapita sehemu mbalimbali,

chipsi enzo hzo shi 5 chips mayai kienyeji humalizi kuku paja shi kumi,mama yaan uhondo tu. basi hapo tu.

demu ukimpa hela nyingi kama shimia 5 hivi hataki atanunu nini. ya nini. ukiona gari mnashangaaaaaaaaaa,, kama ni wazungu manawasalimia hivi , si jioni si mchanga GOOOOOOOOOD MOOOOOOOOOOOOOOOOON Ticher,. wakiwapungia mkono mnafurahii, hapo hatujaoga umeenda barabarani vichafu, tunasubiri wazungu kupita wanaoenda mission/

Bazizane said...

hapa kwenye kuku hata mimi nafagilia zaidi kwani wao ndiyo wanapata kitu fresh na chenye afya zaidi, hao kuku wetu wa China maradhi matupu

Anonymous said...

teh teh hiyo miguu mizuri kwa kufanyia massage janani. maisha haya huyo basi ukute hajui mafua , marali ukimbwi, anakula mlo bora, si baga wala piza, nini maji kwenye mtungi,kibuyu ndo glasi, viatu mzigo kwake yeye tena anawashangaa mnayemuongea huruma, kashazoea hizo raha mkimpa saizi,zitamuaffect na maisha yake halisi, tena raha zenyewe siku hizi za kichina. ukisema ule chakula mafuta mchina kashazingua humo kila kitu na nyie akina shoga wapenda masupermarket, ndo mnaproduce sumu na kuuuwa mbegu za kike na za kiume mavitu yapo modified tayari yamedungwa madawa et nazi ya kopo, maharage,kila kitu nyanya ya wiki mbili imenunda vilevile kama ipo kwenye shila lake we unajidanganya eti nzuri na joto la dar hushangai ipo kila siku haiozi vile wameifunga kwenye packed nzuri,basi tajiri wewe mamam, wa kisasa wewe,kumbe unanunu antvitamini.

kuleni madagaa, kama jide, ma milenda, mayai kienyeji bei rahisi unaenda manzese pale kuku wanakuchinjia mayai trei shi elf 9 kuku ele 8 ukila unamsikia mtamu tena hadi mikupa.

sio kama hawa mabroila wetu unakuta kuku unamchemsha bado anatoa damu mifupani, kumbe wamemuwahisha kufa alijjimezea madawa ya kurefusha maisha, we umekazana kumchemsha mpaka anarojeka.

kijijini hoyeeeeeeeeeeeee, hawa ndo wanfanya sisi tuishi,japo mjini ujanja ujanja wanaleta mazao freshi, sisi unayaweka madawa ya kukaa muda. wakati wao wantegea tule tunenepe tuwafate tena.

sophia said...

Ester kweli mnajionea mambo huko hiyo hali ya kutembea bila viatu inasikitisha kwakweli, ila huyo kuku wa kienyeji namtamani analadha tamu mmnoooooo. Thanks mameii kwa picha , tunasubiri nyingine tukumbushane maana watu wakiwa mjini hapa na life za juu , wanajisahau!

Anonymous said...

mhm jmn kwl tunatofautiana sana kimaisha ila mshukuru mungu kwa hicho alichokupatia pumzi ni zawadi tosha wala huhitaji mbwembwe ila jmn wenye uwezo inabidi kujitolea zaidi kusaidia jamii loh hv jiangalie ulivyo hlf angalia na hizo picha roho haiumi jmn

Anonymous said...

yaani haya maisha raha sana,asikuhadithie mtu,kule kwetu ilembo utakuta mtoto kama huyo asubuhi yupo kifua wazi afu kuna baridi ya kufa mtu lakini yy anakula zake muwa afu hajui cha athma wala babu yake malaria. yaani ndo tz yetu mwana

kai rooney said...

Haya ndio maisha halisi ya mtanzania. Thanks Ester kwa picha.

Ester Ulaya said...

Badi asante, am not a Photojournalist ila napenda sana kushare na wenzangu mambo mbalimbali hasa ya jamii, kwani naamini wengi hasa tuliopo mjini tukikumbushwa kwa picha kama hivyo tunakumbuka tulikotoka na am sure wapo watakaoamua kufunga safari wakasalimie ndugu na jamaa tuliowaacha huko.

Kwa upande wa hewa ni full oxygen hakuna kunyang'anyana hewa

Anonymous said...

hiyo miguu ni timbaland tosha hata msumari haupiti.

Hadj Drogba "mwana chelsea" said...

Hii lazima ni made in SWANGA,nakujua huko,niliwahi kuwa huko nikicheza mpira timu ya ujenzi RUKWA kipindi kile ikishiriki ligi daraja la kwanza(siku hizi mnaiita vodacom premier league)tulikua na kina huyu YUSSUF TIPPO,Msimuone vile mkadhani mtoto mayai jamaa mgumu yule,tulikua nae maisha yale magumu,but those were the days bwana,ligi kuu ligi kuu kweli,sio sasa eti timu moja inashinda mechi zoooote!