Tuesday, September 14, 2010

KAHAWA YA KUPUNGUZA MWILI

Nimepokea mails nyingi sana kutoka kwa wanaume na wanawake wakiulizia sababu iliomfanya Captain kupungua kwa muda mfupi. Ili nao wajarribu

Samahanini kwa ambao sikuweza kujibu mails na SMS zenu.
Sio kwamba nimepuuzia ila wingi ndio umenifanya kuelemewa
Sasa basi nimeona nikijibu kwa blog wote mtasoma na kuelewa na kunirahisihia kazi ya kumjibu mtu mmoja mmoja


Hili ni kopo la Kahawa ambayo tulinunua nchini China baada ya mwenyeji wetu kutuambia kuwa kuna Kahawa maarufu China inayosaidia kupunguza uzito na mwili.
Inawezekana isiwe ni dawa ya Kitambi moja kwa moja, lakini ukinywa unapungua mwili mzima pamoja na Tumbo


Ndani ya Kopo moja kuna vipakiti vidogo vidogo 26, Na ili uone matokeao mazuri unashauriwa utumie makopo mawili "kwa maana hiyo unywe vipakiti 52"
Ni mara moja tu kwa siku. Unaweka kipakti kimoja kwenye maji moto bila kuongeza sukari wala maziwa unakunywa.

Ki ukweli imefanya mabadiliko kwa wiki 2 kabla hata hatujafungua kopo la pili.
Inasemekana haina madhara na imepitishwa na shirika la Viwango nchini China
Inatumika sana North China, ambako ndio kuna idadi kubwa ya wa China wenye miili

Uzuri wa Kahawa hii inapunguza hamu ya kula mara kwa mara na muda mrefu unajisikia kama tayari umeshiba, hata ukila ni kiasi kidogo sana cha chakula.
Ila ukianza kutumia jitahidi maji kwa wingi, matunda pamoja na vyakula vya kuchemsha zaidi visivyo na mafuta.

Epukeni vyakula vyenye wanga hasa nyakati za usiku
Kuwa na nidhami na chakula ni jambo la kuzingatia sana.

Sio unamaliza tu halafu unaenda kufundia KitiMoto, mabadiliko hayaji ng'oo

Watu wameniuliza kama inapatikana wapi na ni sh. ngapi, Kwa bahati mbaya tulileta makopo mawili tu ila kama mtu anahitaji anaweza kuulizia kama ana mtu China amletee, au kama mtahitaji msaada wangu nitaweza kuwasiliana na mtu atakae nitumia hizo Kahawa na mzipate kupitia kwangu.

Unaweza kuniandikia e mail judyjaydee@yahoo.com
Au nitumie SMS 0773 212 000
Kwa watakaotaka kupata kupitia kwangu

Captain Before

Captain After.........jumlishia na kutembea au kukimbia kidogo sio lazima uende Gym.

Hiyo pia itakusaidia zaidi, Punguzeni Bia kwa sana.

Pamoja na yote hayo bidhaa hii inaweza ikakufaa wewe isimfae mwingine.
Ila sio vibaya kujaribu kwani masharti yake sio magumu kabisaaa


25 comments:

Anonymous said...

Thanks kwa information jide. ila me naona eti captain wako hata hakuwa mnene kivilee, hadi kutafuta hio kahawa. ila sio ishu mradi wewe na yeye mmependa. Hope wanaohitaji watafaidika, mwenzenu mie mama wa watoto wawili ila ni kimbaumbau kupita maelezo, kila siku najaribu kula niongezeke hata kidogo wapi. Cheers!!!

Anonymous said...

kitambi chenye kilikuwa wapi jamaa angu ulongo tu

Anonymous said...

kitambi chenye kilikuwa wapi jamaa angu ulongo tu

Anonymous said...

Mamiii thank youu soo much mie ni yule mwenye email ya sexylook65@ymail.com kiukweli nataka immediately agiza kipenzy fasta looh kopo 2 nataka

Anonymous said...

Kwenye picha bado anaonekana hajapungua sana lakini ijumaa nilimuona Mzalendo nikashtuka nikataka kusema anaumwa au amekumbwa na kitu gani huyu jamaa

Anonymous said...

Hello dada Jide even me nahitaji maana hiki kitambi nilichonacho hata nikivaa top natisha pamoja na hizi nyama uzembe utakuwa umetusaidia sana pliz tutajie na bei kabisa mi nitanunua hata nne na mwenzangu pia...email yangu ni veronicajr00@yahoo.com. siku njema!

Anonymous said...

Please Jide hide my email maana nishaanza kutumiwa msg pliiiz

Anonymous said...

Mpenzi jaribu kuhide email za mateja wako watu wataogopa sasa

Anonymous said...

hii ni sehemu ya comments na sio sehemu ya nyinyi kutuma e mail zenu, nadhani mail ya jaydee iko hapo pembeni kama mnataka privacy mngekuwa mnatuma mails na sio kutuma comments halafu mnaanza kulalamika, kazi yake sio kuchuja yale mnayoyapenda na msioyapenda mnampa mzigo wa lawama

Anonymous said...

Jd unamnyanyasa sana mume wako, hakuwa mnnene sema wewe tu hupendezwi nae sio fair

Anonymous said...

Unene sio mzuri kwa afya. Hiyo ni kweli na haipingiki ila naomba tuwe waangalifu sana na hizi kahawa za kichina au vidonge vyao. Hawa watu si wa kuwaamini sana. Nimeshuhudia mtu kapoteza maisha kwa ajili ya kushiriki vidonge vya wachina vya kupunguza uzito. TUWE MAKINI TAFADHALI.

suzie said...

Jide mwenzangu ainidi it raiti nawo and my namba is 0773212000 rinamba rimethajiriwa hiro

Zonda said...

too early kusema haina madhara, tusubiri mpaka ipite at least miezi 2.Naomba utuandikie jina lake kamili wengine tupo mbali tunaweza ku-source toka huku tulipo

Unique said...

Thanks kwa kutujali fans wako my dear, mie pia nataka kopo 4 for me and my hubby, please tupe gharama zake ili tujichange change. Mwanamke mwembamba urembo shost.

Anonymous said...

Ni kitu kizuri sana JIDE unachotaka kutusaidia kwa wajasiliamali hapo wameisha ona "Business Opportunity" I hope wewe ni mmoja wao. Ushauri wangu ili badae yasije tokea yale ya Kuchomewa bidhaa

1. Peleka sample ya kipakiti TBS na TFDA ili waangalie na kuthibitisha ubora wake badala ya kuangalia short benefits alizopata Captain ndiyo ikawa control yako.

2. Tatizo la bongo ni usanii, wewe unaweza ulipata kahawa original ila wajasiliamali wapenda faida watatuletea ma-chemical ya kuyeyusha mafuta mpaka moyo na maini vikayeyuka, Hivyo ukipeleka sample yako TBS itasaidia pia kutumia kama control ya fake zitakazoingizwa baada ya soko kuchanganywa.


Zamani kabisa kulikuwa na chai ya kupunguza unene, nakumbuka kuna bwana mmoja pale Tabora kwa jina la "Sauti ya pesa" alitumiwa ili kupunguza unene akawa anaenda haja mafuta tu na haikuchukua siku mbili akawa ametutoka. So nina uhakika chemical kama hizi bado zina-circulate bongo, hivyo si ajabu baadae watu wakaathirika kwa kahawa fake wakasema ilianzia kwenye blog ya Jide, bado tunaipenda machozi yetu hatutaki wahuni wachukue advantage kwako. Fuata ushauri wangu you will be safe from scavengers wa idea za watu.

Anonymous said...

Mshikaji hizo Rangi rangi ni mchakachuo kwa kwenda mbele, macho yangu yamepofuka lol!!

Anonymous said...

jide unatafuta segerea,utaua watu wakusweke lupango tukose burudani.
tena hawa wabongo wanapenda kudandia magari kwa mbele wameshaanza kuagiza bila kuuliza vizuri.

Anonymous said...

kama unampenda mumewo mweleze afanye mazoezi sio mambo ya artificially kuna magonjwa ya cancer na vitu ambavyo hamna uakika navyo huwezi jua longterm effects zake ni nini mdau wa texas

Anonymous said...

ANGALIENI JAMANI ISIJE IKAWA BAADA YA MUDA MTARIMBO TENA DORO!

Anonymous said...

Wasiwasi wangu ni kwamba kama inapunguza mwili wote, icje ikapunguza hata MAENEO nisiyotaka yapungue!!

Anonymous said...

Mh! mie cpo. mm nilitaka kupungua nilichofanya ni kupunguza msosi, kunywa maji kwa sana, zoezi la nguvu. nimeenda pima kg nimeshakata 3. achananeni na mambo yacyo rasmi jamani, kwani kunenepa ulikula dawa? acheni kuendekeza mambo. wachina noma, ohoo.. ukiwa unadhani unayeyusha kitambi mara kila kitu kinayeyuka INAHUSU? tuwe makini plz.

Gg

Anonymous said...

Kunyweni tu mzidi kuota ndevu

Anonymous said...

Jide, me sijawahi kuingia machozi band bt I am fan of ur blog, shemeji hakuwa mnene, he had manly lovable body, sasa kawa kama mtt! Naona hajapendeza hata, kama naumwa vile, pika tena arudie ule mwili wake, was ver nice

ald said...

mbona hujataja bei?
mie nataka pia

Anonymous said...

msituchoshe bana na miji maneno yenu ushauri ushauri, sisi wote ni watu wazima na kila mtu ana maamuzi yake akiamua kunywa au kufanya mazoezi sasa kama nyie hamtaki mbona mnataka kutupangia maisha na wengine. sisi hatuwezi mzoezi kwa kifupi ni wavivu na tunataka hiyo kahawa