Saturday, August 13, 2011

NIMEPATA DIET NYINGINE RAHISI YA KUPUNGUZA MWILI NA TUMBO LA CHINI KWA WANAWAKE....Inaenda kwa mwezi mmoja" Ukipenda kufuatilia tuanze wote leo"

Kuna njia nyingi sana ambazo watu huwa wanajaribu ili kupunguza mwili na tumbo lakini either zinakuwa ngumu sana au zinakuwa haziendani na mazingira wanamoishi hivyo kupelekea kushindwa njiani.

Zipo njia za kutumia madawa kama kahawa na vinginevyo ambazo huwa si za kudumu.
Kwakuwa kahawa huwezi kutumia zaidi ya round 3 kwa maana hiyo ukinenepa tena inabidi utafute njia nyingine.

Lakini njia hii ifuatayo unaweza kuifanya ikawa ni maisha yako ya kila siku ikazoeleka na ukawa unaishi hivyo hivyo bila kuongezeka mwili.
Mara nyingi vyakula tunavyokula na vinywaji tunavyokunywa ndio vinatuponza

Sasa, je! Unaweza kujaribu kuishi hivi bila ku cheat hii process???


Siku ya kwanza, ukiamka tu kitandani ukapata nguvu kabla ya kufanya chochote jivalie raba zako na nguo za mazoezi. Jaribu kutembea dakika 15 toka nyumba unayoishi na dakika 15 kurudi nyumba unayoishi hapo jumla utakuwa umetembea kwa miguu kwa dakika 30.


Na kama mkakati wako ni kupunguza Tumbo pia, Ukirudi fanya sit-ups 15 -20 kwa siku ya kwanza. Ukiona ni ngumu unaweza kujaribu kuanza hata na 10. Utaongeza kadri siku zinavyoenda na kadri utakavyokuwa unazoea maumivu ya nyama za mbavu.

Unaweza kutumia Bench au unaweza kulala sakafuni
Kwa wanaoishi Dar es Salaama ma bench ya Sit ups yanapatikana Shopperz Plaza kwenye duka la vifaa vya michezo

Ukimaliza kutembea na kufanya sit-ups kunywa maji ya uvuguvugu glass 4
Sio lazima uyanywe yote kwa wakati mmoja
Unaweza kuwa unakunywa huku unaendelea na mambo mengine mpaka glass 4 ziishe
Ili kuongezea ladha unaweza kukamulia ndimu au limao katika maji hayo ya uvuguvugu

Limao na ndimu sio tu huongeza ladha bali pia vinasaidia kupunguza mafuta mwilini

Baada ya hapo unaruhusiwa kwenda kuoga, na kujiweka sawa ila usipige mswaki
Nitakwambia kwa nini!!

Kunywa breakfast yako:
Unaruhusiwa kunywa kikombe 1 cha kahawa au Chai lakini usiweke zaidi ya kijiko 1 cha sukari
Unaruhusiwa kula yai 1 tu la kuchemsha

Mikate hii ya brown mimi siipendi na wala haina ladha nzuri lakini utafanyaje maadam unataka lako la kuepuka unene yabidi ule tu.

Slice 1 tu ya brown bread tena iwe toasted, usithubutu kuweka Siagi wala vinavyofanana na hivyo
Matunda jimiminie kadri uwezavyo, epukana na ndizi tamu
Baada ya hapo unaweza kupiga mswaki sasa na kuendelea na shughuli zako
Ila kabla ya kuendelea na shughuli zako ni lazima utaenda haja kubwa
Ndio lengo hasa la kutopiga mswaki kabla ya breakfast

Lunch:
Kula upande wa kuku Robo, 1/4 my friend kama ni upande wa paja ndio uliochagua
Kuku unaetakiwa kula ni lazima awe wa kuchoma au kuchemsha na si vinginevyo

Ukitaka upande wa kipapatio ndio utakao kuwa umeuchagua pia.
Unaruhusiwa kusindikizia na kachumbari/ au hata Salady zenu za kizungu za mahotelini
Kama ukiona hujashiba kunywa maji.
Bold
Kumbuka lengo sio kushiba bali kupunguza mwili.
Baada ya hapo ni lazima unywe tena maji ya uvugu vugu glass 4

Epukana kabisa na maswala ya juice zenye sukari nyingi
Mida ya jioni jua likishazama baada ya kazi ukirudi nyumbani, au kama utakuwa umebeba nguo za mazoezi kwenda nazo kazini. Unaweza ukatembea tena kwa nusu saa
Halafu ukamalizia na sit ups ukingoja Dinner

Ukishaoga jioni.
Huu ndio uwe mlo wako wa kufunga siku "Supu ya Samaki"
Samaki wa aina yoyote tu ile weka bakuli kubwa la kutosha.
Ila pia, hakikisha supu hiyo ni chuku chuku na haina mafuta wala viazi hata kidogo

Nikutakie siku njema na majaribio mema
Tukutane tena Day 2:
Kama kweli una nia
Hii ngoma inaenda mwezi mzima

KUMBUKA PENYE NIA PANA NJIA

14 comments:

Anonymous said...

Duh hii kitu nimekuja kuisoma late tayari nimeshatandika vitu vizito huko tumboni labda nitaanza kesho ila Leo nitajaribu kula matunda na hayo maji kwa siku iliyobakia jioni nitajipiga gym. Thanx for the tips Jide

Anonymous said...

JIDE HAPA MIE NAKATAA KABISA NAONA KAMA UNAFANYA UPENDELEO FLANI HIVI SISI NI MASHABIKI WAKO NA NI KWELI TUNAVITAMBI KWA NINI HII KITU USISUBIRI HAD RAMADHANI IIISHE JAMANI TUANZE WOTE SIO WOTE MAKOBE KAMA WEWE

PLZ KWA MSAMAHA WAKO KATISHA HII KITU BANA TUANZE WOTE BAAD IKISHAPITA SITA NA IDI YA SITA TUKIMALIZA TUANZE DIET WOTE HII UTAKUWA HUTUTENDEI HAKI NASIE TUNATMANI TUFANYE ILA TUKO KWENYE MFUNGO NIWIE RADHI SANA MAMII KAMA NITAKUWA NIMEKUKWAZA AM JUST SAYING

MREMBO

Anonymous said...

Naungana na wewe kabisa hilo ndio suluhisho la kudumu, mazoezi pamoja na mfumo wako wa kula vinginevyo ni suluhu za muda mfupi sana na rahisi kukata tamaa.

Thanks Jide.

kai rooney said...

Hii diet naona inanifaa lakini kabla sijaanza inabidi nijipe mazoezi kwanza ya kutembea na kunywa glass 4 za maji, hii ndio kazi kubwa kwangu nilioiona. Asante mamii.

Anonymous said...

jay dee asante sana kwa diet nafurahi sana unawapa watu moyo. watu wanasema mpaka wamalize mfungu unajua kama kufunga ni diet tosha ukifuturu kula chakula kidongo kama alivyoandika itasaidia sana sio mpaka umalize kufunga. please tunaomba tuandikie ya kuendelea maana tumesha anza hii pamoja na kwamba tumefunga asante sana mungu akubariki.

Anonymous said...

Acheni kuwa selfish, sio kila mtu ni muslim vipi kwa sisi ambao hatufungi wa madhehebu mengine na tunahitaji? angalia wewe unaemuita mwenzio kobe usije kuwa wewe ni nyoka tu

Anonymous said...

nina tumbo la juu jide na linaniboa kinoma cwezi hata kuvaa top, help plz!!!

mama siyabonga said...

duuuh jide hapa tupo pamoja haswaa mie naanza kesho asubuhi na mapema..thank girlfriend

Anonymous said...

asante dear kwa diet nzuri ila swali sasa kwa tunaonda kazini asubuhi tutapigaje mswaki may dear?

Anonymous said...

mbona kuhusu mswaki pia imeandikwa soma vizuri August 15, 2011 2:27AM

Anonymous said...

hakunaga cha mfungo, waislamu wamebadili muda tu tazama; jioni/futari=breakfast/chai asubuhi, saa5 msosi=lunch na saa 10 alfajiri msosi=dinner ya saa2-3, so hakuna cha mfungo hapo,dini siasa tu.

Anonymous said...

Sasa wewe umefunga alafu unamuita mwenziyo kobe itakua unashinda tu nanjaa or unafuata mkumbo tu thankx Jide tupopamoja sana usiachekuandika nakuomba

Anonymous said...

Sasa wewe umefunga alafu unamuita mwenziyo kobe itakua unashinda tu nanjaa or unafuata mkumbo tu thankx Jide tupopamoja sana usiachekuandika nakuomba

ngaizaskids said...

asANTE JIDE naanza leo kupunguza tumbola uzazi japo nimechelewa. pamoja.

Kokusima