Pages

27 January 2012

BAMIA YA NAZI KWA HATUA


Ignore hilo Limao linaloonekana kwenye picha halihusiki kwenye hii mboga

MAHITAJI:
Nyanya, Vitunguu, Mafuta ya mimea (Veg oil), Chumvi, Nazi na Bamia
vilivyokatwa katwa kwa muundo unaoonekana hapo juu


1: Unakaanga nyanya na vitunguu pembeni mpaka vilainike na kuwa rojo zito
2: Unaweka mafuta kidogo sana kwenye sufuria/kikaango kisha unaweka bamia zilizo katwa na kuoshwa vizuri
Unazigeuza mpaka uone ule udenda wake umekata na haupo kabisa

3: Ile hali ya bamia kuvutika kama big g ikiisha isha unamimina mchanganyiko wa Nyanya na Vitunguu ulivyokuwa umekwisha viandaa mwanzo, unaacha ichemke na kuchanganyika kwa dakika 1

4: Baada ya hapo unaweka nazi ya aina yoyote inayopatikana karibu yako
Iwe tui fresh, au za madukani Coconut Milk/Cream pamoja na chumvi
Unaacha ichemke na ichanganyike kwa dakika 1

Baada ya hapo mambo yanakuwa tayari kuliwa
Utaamua unataka kula na Wali, Ugali, Chapati, Mkate n.k

15 comments:

Anonymous said...

Nmhhh duhh Jide Shemji G.H anafaidi kwa misosi ya namna hii,,,sasa muda huu uko Majuu unamwacha vipi Bwana Mkubwa?

Anonymous said...

inavutia

kai rooney said...

Hili pishi linanihusu. Thanks

monica kaaya said...

Iyoleo lazima nikaijaribu asaaaante sana kwakunipa ufundi wangu

Ester Ulaya said...

yaani hapo nitakula kwa ugali au wali, tamuuuuuuuuu

Jestina George said...

Hii lazima niipike

lyna wa ukweee said...

mhhhhhhhhhh namezea mate kwanza mna yameshajaa kuona ilo lost hapo,ongra dada uko juuuuuuuuuuu.

Anonymous said...

Asante kwa kutufundisha hili pishi Jide, nitaenda kulipika na mimi nyumbani.

mama siyabonga said...

Mmmmmh jide yaani ni yam yam kwa sana...jinsi ninavyopenda bamia hiii lazima leo leo niifanyie mambo then nijipe utamu..
Ahsante kwa kutuletea kitu roho inapenda.

Eunice said...

kweli tembea uone, najuaga km hizi bamia huwa zinangwa kwa nazi lakini za kukata kata ndogo ndogo ndo nimeziona hapa na nimezitamani, kesho mungu akipenda nitazikorofisha, maana zinaonekana tamuuuuuuuuuuu

Anonymous said...

Mafuta unaweka kama kiasi gani jide? vijiko vikubwa vingapi maana mimi huwa ni mbvu sana kwenye swala la mafuta nikipika nyumbani wanalalamika nimeyajaza

annette said...

sweeet thanks uwe unatuletea haya mambo often wengine ni wamasi hatujui mazaga zaga mama!

Anonymous said...

Nnavyochukia bamia, sijui...ngoja nijaribu kwa mtindo huu labda nitaweza.

Matola said...

Mmmh! hadi mate yananidondoka hiyo lazima niitengeneze tena sasa hv!

missy said...

Aisee pishi ni tamu hili kwa ugali...thanks Jide I went and tried it