Sunday, June 17, 2012

AJALI YA TRENI ILIMKUTA KIJANA WA MIAKA 17, MUNGU AMREHEMU


Kijana mdogo wa miaka 17, Jackson Thobias aliyekuwa akisoma kidato cha nne ESACS Academy, amefariki kwa kugongwa na treni maeneo ya kwao kipawa, aligongwa akiwa anasikiliza music kwa headphones huku akichati katika simu yake wakati akitembea kwenye reli.

Pamoja na mlio mkubwa wa treni, na juhudi za watu kumpigia kelele kuwa kuna treni inakuja nyuma yake, Jackson hakusikia.

Marehemu Jackson ndio aliye shinda kwenye Tokelezeiyer Inter-School concert iliyoandaliwa na group  ya Friends 4 Friends tarehe 12 may 2012, pia alishinda dougie competition  wakati 5select Event ya EATV ilipotembelea ESACS wiki mbili zilizopita.

Alikuwa ni kijana mwenye kipaji na ndoto nyingi katika umri mdogo wa miaka 17, Mungu aipumzishe roho ya marehemu Jackson Thobias kwa amani, Amen.

Habari na picha toka kwa ZAINUL wa MO Blog

2 comments:

Anonymous said...

Inasikitisha sana, nawapa pole familia ya marehemu na wale wote walioguswa na msiba huu. Mungu ailaze roho ya marehemu peponi Amen.

Anonymous said...

Dada asante kwa habari kama hii, lakini ushauri tu si vizuri sana kuweka picha cha maiti zikiwa wazi ujue it pains hata kuumiza zaidi kwa watu

Deliwe