Sehemu wanayoishi watoto hao wenye ni sehemu ambayo mazingira yake sio ya kuridhsha kabisa
Kwa mtu yoyote akifika hatasita kutokwa na machozi
Hii ni njia ya uchochoro ambayo inaelekea kituoni hapo
Gari haiwezi kupita hivyo ilitulazimu kupaki barabarani na kutembea kuelekea kituoni, kama inavyoonekana kwenye picha
Huyu mama ndio mlezi wa kituo hicho
Pamoja na hali duni iliopo kituo hicho walijitahidi kupamba na kutuandalia mazingira tujisikie kama wageniWatoto wengi ni wenye umri mdogo sana ambao wanahitaji malezi na uangalizi wa hali ya juu
Beautifull
GK akisaidia kushusha vyakula vya msaada kituoni hapo
Nyumba wanamolala watoto hali yake si nzuri hata kidogo
Vitanda ni vichache kwahiyo huwalazimu kubanana
Happy Happy
Wanty
Maggie Musa na Leon Lee
Sab
Wise Monica Kaaya
Tulijikuna mpaka hapa japo kuna mengi wanayoyahitaji zaidi
Faraji
Binti alisoma risala ilioelezea matatizo wanayokumbana nayo kituoni hapo
Sisi kama LA FAMILLE hatukwenda kituoni hapo kwaajili ya show off bali waliniandikia barua ya kuomba msaada nami nikaona ni vema kusaidiana na wenzangu.
Na wanahitaji kutangaziwa zaidi ili watu wengi wajitokeze kusaidia kwani hali yao ni tete ki fedha na kimahitaji
Baada ya kusoma risala hiyo fupi alinikabidhi
Nili play part yangu mpaka hapa ila kwa bahati mbaya nasikitika kuwa sikuweza kukaa muda mrefu na kula chakula cha mchana pamoja na watoto hao kutokana na kuwa ilinibidi niwahi airport kuelekea BUNDA kwa mazishi ya bibi yangu.
Lady Jay Dee na baadhi ya wanafamilia wakipiga makofi baada ya risala kusomwa na mtoto Khadija Mussa (hayupo pichani).
Lady Jay Dee akipokea risala kutoka kwa mtoto Khadija Mussa.
Lady
Jay Dee akikabidhi msaada uliotolewa na Familia yake vikiwemo Mchele,
Maharage, Mafuta ya Kupikia, Sabuni za Kufulia, Nguo, Juisi pamoja na
vingine vingi. Anayepokea msaada huo ni Mlezi wa Kituo hicho Bi.
Zainabu Bakari (kushoto) pamoja na mmoja wa watoto wanaolelewa katika
kituo hicho Khadija Mussa.
Jay
Dee Family inawakaribisha wadau wote watakaoguswa kutoa mchango
chcochote walichonacho kupitia Jay Dee Family. Kwa mawasiliano zaidi
wasiliana na Judyjaydee@yahoo.com.
Lady Jay Dee akibadilishana mawazo na walezi wa kituo hicho baada ya kukabidhi msaaada huo.
Mwanafamilia Ester Ulaya (kushoto) akiteta jambo na Komando Binti Machozi Lady Jay Dee.
Pichani
Juu na Chini Wanafamilia wa Lady Jay Dee wakipakua chakula
kilichoandaliwa Nyumbani Lounge kwa ajili ya kula pamoja na watoto
yatima wa kituo cha Maunga Centre.
Watoto wa kituo cha Maunga Centre wakipata chakula cha mchana kilichoandaliwa na Jay Dee Family.
Vijana wa Jay Dee Family wakiwajibika kuhudumia chakula kwa kituo cha kulelea watoto yatima cha Maunga Centre.
Mlezi
wa kituo cha Maunga Centre Bi Zainabu Bakari ambapo amezungumzia
changamoto zinazowakabili ni sehemu ya kuishi wahudumu wa kituo hicho,
mishahara ya kuwalipa wahudumu na makazi ya wahudumu wa kituo hicho.
Bi.
Zuhuru Bakari alisema kituo hicho kinalea watoto 30 ambapo watoto 20
wanalelewa nje ya kituo kwa baadhi ya walezi waliowachagua wao kutokana
na ufinyu wa eneo jumla yake inatengeneza idadi ya watoto 50.
Mwanafamilia
Ester Ulaya akizungumza kwa niaba ya Jay Dee Family ambapo amesema
watakuwa bega kwa bega na kituo hicho na kuendelea kuwatafutia wafadhili
wa kusaidia kituo hicho.
Baadhi ya wanafamilia katika pozi na walezi wa kituo hicho.
Wanafamilia katika picha ya pamoja na walezi wa kituo hicho pamoja na watoto yatima wanaolelewa kwenye kituo hicho.
Zainul Mzige wa MO BLOG alijumuika na Familia ya Jay Dee katika kutoa msaada kwa watoto yatima wa kituo cha Maunga Centre.
















17 comments:
mungu akubariki jide azidi kukuongoza kwa kila jambo
JIDE UMEFANYA KITU CHA MAANA SANA KUWAKUMBUKAWATOTO YATIMA. ALLAH ATAKULIPA ZAIDI YA HAYO. BUT NINGEOMBA UMCHUKUE MTOTO 1. UMLEE MWENYEWE, ITAPENDEZA SANA MPENZI NI MAWAZO TUU.
hongera sana dada yangu kwa upendo ulionao natamani na mimi niwe kama wewe, mungu akubariki sana
jane L
hongera sana la familia.mungu awaongezee pale palipopungua.
Kazi nzuri kabisa mliyofanya La Famille,Mwenyezi Mungu awabariki na kuwazidishia pale mtakapokuwa mmepungukiwa ili mzidi kuwa na moyo huo huo wa upendo na mshikamano.
mungu akubaliki sistee jide komando. much respect sio kaa hoa supa staa wengine wala vumbi kila kukicha wanauza sura kwa skendo huko gpl.
big up La Familia, mungu awazidishie kwa kila jambo, missing u, panapo uzima tutaonana mana majukumu yamebana, stay blessed all.
La famillia mmethubutu na mmeweza, Mungu awarudishie pale mlipotoa.
Napenda kukwambia kitu mama wa la Famille. Utabarikiwa kila iitwapo leo maana Wewe ni mtu zaidi ya mtu kwani mtu ni utu na wewe unao huo utu. KILA la kheri katika maisha yako yote.
huo ndio umoja wenye maana kuliko hata kuparty.Mungu awarudishi na kuwazidishia pale mlipo toa. kumba maneno ya mungu yanasema kulisha wajane na yatima ni kumkopesha Mungu.
Rida
jmn watto kweli wamefurai mbarikiwe na mungu awajalie zaidi ya hapo mna mmefanya kitu kikubwa sana ktk jamii yakuwakumbka hao watto
congrats sana maana ndo mikuwakumbuka nyie tunahisi km na sisi tumewakumbuka japo hatujatoa chcht lkn kwa maombi wapo pmj na sisi! hongera sana kwa kuwa na moyo wa huruma na wakusaidia watoto hao naimn mungu atakuongezea pale ulipotoa ubarikiwe sana
Mungu wazudushie pale mlipotoa. Familia nzuri sana nimeipenda, Mungu akijalia tutaonana soon!!
Ukiziangalia sura za watoto pamoja na matatizo walionayo wanaonyesha walifurahi hizo ni baraka zaidi kwenu Jide
well done ma dear
Well done...sio kwenda kutoa pesa na kufanya mabonanza kwa ajili ya kunywa pombe tu. Be blessed...!!!!!!!
GUD JOB LA FAMILIA,INGAWA WENGINE BADO TUPO MBALI ILA MNATUWAKILISHA VEMA SANA.BIG UP DADAA JIDE,WE LOVE YUUU!!!
Post a Comment