Ndugu Mgeni Rasmi
Maunga Centre ni kituo cha kulelea watoto yatima na waishio katika mazingira magumu.
Kituo kimeanzishwa mwaka 2008 na kusajiliwa mwaka 2011
Kituo kina watoto 50, kati yao 30 wanaishi hapa kituoni na 20 wanaishi na walezi wao.
Lakini mahitaji ya kibinadamu wanayoyapata hapa kituoni, Sisi kama viongozi wa Maunga Centre hatupendi watoto hawa kuishi na walezi wao, ikizingatia kuwa hawana uwezo ila kutokana na uchache wa Vyumba imelazimika iwe hivyo.
Uongozi wa Maunga Centre unatoa shukrani za dhati kwa kukubali wito wetu wa kuja kuwatembelea na hii inaonyesha jinsi gani unavyopenda jamii bila ubaguzi.
Maunga Centre ilituma barua kwako ya maombi ya kuwatembelea watoto hawa yatima ambao hawakupenda kukosa wazazi wao. Tulituma maombi kwako kwasababu tuna imani kubwa kuwa wewe ni kioo cha jamii na mpenda jamii bila ubaguzi wa rangi, dini, jinsia, wala ukabila wewe ni mtu wa watu wote.
Kitendo ambacho leo umekifanya cha kuwatembelea watoto na kula nao chakula pamoja ni kitendo cha kihistoria kwa jamii ya Watanzania na tunaamini umefuata maagizo ya Mungu kwa dini zote.
Tukumbuke kuwa tendo la kuwatembelea yatima, kuwasaidia, kuwafariji kwa kuondokewa na wazazi wao ni ibada au sala kubwa sana kwa Mungu
Tunawashukuru wote ambao umeungana nao katika msafara wako sisi kama kituo tunasema hatuna cha kuwalipa ila malipo mtayapata kwa Mungu, pia tunawaombea Mungu awape uzima, kipato na awapandishe vyeo uko kazini kwenu ili kipato kiongezeke muweze kusaidia jamii hususani yatima.
Maunga Centre inatoa shukrani kwa misaada ambayo mmetuletea. Kituo cha Maunga Centre kinawaomba MR.&MRD GARDNER kuwa walezi wa kituo hiki,
Tunawaomba kuwa walezi kwakuwa tunaamini kitendo ambacho leo mmekifanya inaonyesha jinsi gani mlivyokuwa na uchungu na swala zima la yatima.
Tunaamini kuwa kutoa ni moyo na wala si utajiri kwasababu wapo wenye uwezo mkubwa lakini hawajitoi kusaidia jamii kama ulivyofanya leo.
MAUNGA CENTRE ina changamoto zifuatazo:
1. Kukosa fedha za kuwalipa wahudumu
2. Kukosa eneo kubwa la kujenga kituo
3. Kukosa wafadhili
4. Watoto hawana sare za shule
5. Kukosa gharama za kuwasomesha (michango ya shule)
Tafadhali tunakuomba ututafutie wafadhili wa ndani na nje ya nchi ili tuwasaidie na tuna imani kubwa kuwa unawafahamu watu ambao wana moyo wa kutusaidia wa ndani na nje ya nchi.
Tunakuomba utusaidie kukitangaza kituo katika vyombo vya habari ili watu wenye moyo watusaidie.
Sisi kama kituo hatuna uwezo wa fedha za kugharamia gharama za matangazo.
Ndugu mgeni rasmi tunakuomba tamasha moja la muziki la kuchangia fedha kwaajili ya kituo cha watoto yatima. Tunakuomba malipo utayapata kwa Mungu.
Mwisho tunakutakia maisha mema, Mungu akupe roho ya imani pamoja na kipato kiongezeke zaidi akupe kizazi chema ambacho kitajali jamii kama ulivyo wewe mwenyewe
Ahsante
Karibu tena Maunga Centre
BINAFSI NINGEPENDA KUANZA NA KUWATAFUTIA KIWANJA KIKUBWA KWAAJILI YA KUJENGA KITUO KINGINE. WAHAME HAPO WALIPO, WANABANANA SANA NA NI VYMBA VIWILI TU AMBAVYO VINA HALI MBAYA SANA.
AKITOKEA MTU WA KUTUSAIDIA KIWANJA, TUTACHANGISHA FEDHA ZA KUANZA UJENZI:
Mimi kama JAYDEE natoa wito kwa yoyote mwenye moyo kuungana nami katika swala hili.
Ikiwa mimi na Gardner tumeombwa kuwa walezi wa kituo hicho, Pamoja tunaweza
Natanguliza shukrani:
JIDE
Hivi ndio vitanda wanavyolalia watoto hao.
Watoto wako 30 na vyumba viko 2
Sasa fikiria ni wastani wa watoto 15 katika kila chumbaHakuna mtu yoyote ambae angependa kuishi katika mazingira ya namna hii, huruma ndio inayohitajika hapa
Hili ndio eneo wanalotumia kama jiko la kupikia chakula
Na hii ndio sehemu ya kujisaidia "CHOO"
Fungua moyo wako, tafadhali i beg you pipo
Haya sio maisha watoto wetu wanayostahili kukulia
Tusaidiane kujikwamua katika umasikini ili hata wakienda shule waweze kufikiria masomo na kufanya vema




7 comments:
Uko juu Jide!......
Mungu akubariki judith. Nimefurahi mno kwa ulichofanya kwa hao watoto. sina tabia ya kucomment lakini leo nimeona nikupongeze.
Ni baraka sana kuwakumbuka yatima au wajane kwani hawakupenda kuwa yatima na hatujua kama sis siku moja nini kinaenda kutokea tutakapokuwa hatupo ni vipi wanetu watakuwa watakapoitwa yatima. Mungu abariki kila atakayetoa chochote kwa ajili ya watoto hao. Huo ndo usupastar halisi jide kuwakumbuka wengine mungu anapokubariki.
Mungu wetu ni mwema sana akikupa uwezo kidogo shiriki na wengine ili nao wapate furaha ktkt maisha yao nomba kujiunga nyie ktkt kuchangia kidogo nilicho nacho. ili kunipata naomba tuwasiliane kwa wankobaf@yahoo.com napatika hapa dar.
Rida
Mungu akuzidishie Jide na wote wana Familia mliojitoa kwa kila hali. Amin
mungu hakubaliki uzd kuwa na moyo mkunjufu wakusaidia kwa moyo dada.
Trust me Judy, Mungu atakufungulia mambo yote yaliyokuwa magumu kwako maan umewajali yatima hao.Be blessed!
Hongereni sana kwa moyo mliouonyesha kwa kwenda kuwatembelea hawa watoto, mimi pia nilitamani kuwepo ila Nimjifungua nipo likizo kwa muda,
Ushauri kwako Jide, Sajili number za simu ili watu waweze kutuma pesa kwa anayejisikia kuchangia pesa, kwa wale wanaotaka kuchangia vifaa basi utawapa utaratibu maalum.
Post a Comment