Saturday, July 21, 2012

IANGALIENI HII, SIJUI MTAITAFSIRI VIPI?? ILA MIMI IMENIFANYA NIJISKIE VIBAYA

Nilikuwa nimekaa nakula chakula, Ndani ya Restaurant moja hivi inaitwa PRIMI
wakaingia wazungu ambao kwa hisia nadhani waalikuwa ni familia moja, kama sio marafiki, katika kundi lao waliongozana na wasichana wawili wa kiafrika ambao wanaonekana dhahiri walikua sio wa mjini kutokana na matendo yao.

Kila mtu mle ndani alikuwa anageuka kuwaangalia kwa kuwashangaa, nikiwemo mimi manake sikutegemea, kitu cha namna hiyo kingeweza kutokea pale Restaurant
wasichana hao hawakukaa juu ya viti kama wateja wengine wote, bali waliomba mito ambayo waliiweka chini wakakalia.
walionekana kuwa busy kuchagua menu ambayo sina hakika sana kama walikuwa wanaweza hata kuisoma,   
na walifanya hivyo bila kujali macho ya watu.

Ila wenzao waliokuja nao walikaa juu ya viti.
Nilielewa kuwa itakua ni mila na desturi zao ndizo ziliwapelekea kufanya hivyo, lakini pia nilijiskia vibaya kuwaona wamekaa chini wakati watu wengine wote wakiwa juu ya viti
Hizo ni hisia zangu, zinaweza kuwa sio sahihi pia
Cha kushangaza zaidi chakula kilipokuja mezani, wengine wote waliwekewa kwenye sahani za udongo....Lakini cha kwao kiliweka kwenye vyombo vya mbao mfano wa tray
Na style waliokua wanaitumia kula ni style mfano wa wanyama na sio binadamu....
Maana walipiga magoti wakainama wakaanza kula, kama vile wanavyokula wanyama....
GlaSS zao za Soda pia chini Sakafuni

Nilijiuliza tu, hao walioongozana nao walishindwa kuwaelekeza jinsi ya kula kama wanavyokula binadamu wengine????
Angalau tu wanapoongozana nao kwenye sehemu zenye macho ya watu wengi wenye tamaduni tofauti??

Hata ukienda nchi za kiarabu unajifunika, hata kama sio Muislam kufatisha mila zao.... 
Ingawaje mwisho wa siku kila mtu atadumisha mila na desturi zake
Nawasifu kwa mavazi, walipiga kitu cha kama Khanga hivi, Na pengine niwasifu pia kwa kulia chakula chini na kwa mikono manake hata sisi tunakula hivyo, ila sio kwa style waliotumia kula kama wanyama...Chakula chenyewe pia walishindwa kula hata robo ladha haikuwakolea

Niliomba kuwapiga hizo picha tu, sikuweza kuendelea zaidi ya hapo niliogopa

32 comments:

kai rooney said...

Inawezekana kuwa hao wazungu wamewaelewesha na hao wenzetu wakakataa so hawawezi kuwalazimisha! ila hilo la kula kama wanyama na mimi pia limenishangaza! sijui wametoka nchi gani!! na kitu kingine ni vipi kuhusu mawasiliano je wanaelewana? maswali ni mengi wewe pia huwezi kutujibu. Thanks kwa kushare nasi.

Subi Nukta said...

Kama kuna somo walikuwa wanataka kulitoa hapo, mimi nimetoka kapa, bado sijalielewa. Nadhani kutakuwa kuna utafiti wa masuala ya sayansi ya kijamii wanadodosa na kuona watapokelewa vipi au jamii inachukulia vipi suala hilo katika tamaduni. Naweza nikawa nimekosea, ila ndivyo ninavyowaza kwa sasa. Nahisi wapo kwenye 'study' fulani wanakusanya 'data' kwa ajili ya 'analysis' baadaye na huenda kuna anayerekodi 'reaction' ya watu bila watu wenyewe katika eneo hilo kujua.

Jide said...

Nilijaribu kuuliza kwa wahudumu na Manager lakini hakuna alieonyesha kufahamu chochote juu ya swala hilo, ulichoandika Subi kinaweza kuwa na ukweli.

Anonymous said...

Kwakweli ningekua ni mimi lazima ningeongea kidogo na hao waliokaa kwenye viti nijue kidogo kuhusu wao. Nisingeweza kutoka hivi hivi kingenisumbua sana (this is just me). Subi anaweza kuwa sahihi, Kai pia anaweza kuwa sahihi. On the other hand hao wazungu inawezekana wanaishi na hao wasichana toka wakiwa wadogo na wanawa-treat kama wanyama huko nyumbani. Kama walichukuliwa wakiwa wadogo na wakawa wanafugwa kama wanyama i.e. kupewa chakula kwa staili hiyo etc hawawezi ku-act tofauti kwenye public. Inawezekana kwa miaka yote hakuna aliyewauliza hivyo na wao hawajali. Kwakweli imeniuma sana nimefananisha na true story fulani nilioyoiona. I hope this is not. I so hope am very wrong on this. God Bless them!

Ester Ulaya said...

hiyo ya kula kama wanyama imeniacha hoi....halafu wanaonekana wako busy sana na simu....Subi waweza kuwa sahihi...kwani hao wazungu wao wako pia busy na shughuli zao, kuna namna hapo sidhani kama kuna tamaduni zetu africa watu wanakula kama mbuzi, sijawahi sikia kabisaaa......labda kama ipo siifahamu...pia wanaongea lugha gani hao?

Anonymous said...

Tudumishe mila na tamaduni zetu ila wakati mwingine waafrika tunazidisha mie naishi ulaya baadhi ya weupe hutuchukulia sie kama watumwa kutokana na ujinga wa watu wachache .Mie nilikaribishwa chakula kwa mweusi mwenzangu ila sio MTZ tulikua tunakula nyama za kuchoma Mume wake anakula nyama anasevu mifuta mdada anachukua anakula . Tulikua wengi nilivumilia mwisho nikashindwa nikauliza akajibu hukumbuki afrika tunapenda kutafuna mifupa. nikamwambia siutafune unayokula ktk nyama uloishika . akajibu mumewangu kazoea hata tukiwa hotelin ni oky mi sijali nimetoka afrika . mara akipiga story anashusha thamani UAFRIKA.anasema fikiria tungekua afrika saa hizi tumetoka kuchota maji ndoo kichwan.vitu kaa hivi tusingeviona sielewi USHAMBA :KUJIDHALILISHA AU NDO AMETOKA KTK FAMILIA MASIKINI KUPINDUKIA AU HAKUTEGEMEA KUFIKA ULAYA SIKUPATA JIBU NA SITAKI KUWA NAE UKIMWELEKEZA ANASEMA SIE NI WAAFRIKA BWANA HATUFIKII WAZUNGU

Anonymous said...

Io ni kali.ila nafkri wana lengo la kufanya ivyo co bure.leon lee

cally said...

inawezekana wapo kwenye research tuu. sidhani kama kuna watu ktk mazingira ya uhalisia wanafanya hayo waliofanya hao ndugu..hata mimi nyama ya mfupa nikiona imeliwa kihasara hasara naivamia...lol ila hayo maelezo ya kuwa afrika tunapenda mifupa nitayaweka pending. hapo lazima nitakuwa nimekaa hapo restaurant na watu niliowazoea,hivyo sio big deal :)

Somebody Not Hater:.... said...

We nawe umeenda kula au kushangaa watu?........

Suzan said...

SOMEBODY NOT HATER, LET ME CALL YOU SOMEBODY HATER. JAMBO KAMA HILO WEWE USINGESHANGAA AU UMESHAONA KILA KITU DUNIANI? INABIDI TUKUSHANGAE KWA KUTOKUSHANGAA.

Anonymous said...

Nakubaliana na mawazo ya wanaodhani wanafanya research fulani sidhani kama inawezekana katika mazingira ya kawaida. Pia anony July 21, 2012 10:26 PM nakubalina nawe kaisa kuhusu baadhi ya tabia za wenzetu wakiwa ughaibuni sijui wanadhani kwa kufanya hivyo ndo watapata misasda au vipi! hata siwaelewi. Kuna mmoja hata aliwahi kusema nyumbani Tz kunanuka kuchafu sirudi tena! kweli!!!

Anonymous said...

"WHAT WILL YOU DO?".. kuna kipindi huku kwao wanafanya mambo ya ajabu kwa watu na kuona watu watahamaki vipi na hicho kitendo hasa huwa wanapenda kuonyesha upande wa ubaguzi wa rangi na utaifa. Sasa kama kitakuwa ni hicho au aina ya kipindi kama hicho dada yangu wewe na wote mliokuwamo humo ndani mtaonekana hamjali na mnaukubali utumwa kwa kumuona mzungu ni bora zaidi kuliko ndugu zenu weusi kwa kutojali yaliyotokea. Sidhani ila kitendo cha wewe kupiga picha na kutowauliza chochote nahisi ndio kimeharibu kila kitu kama kitamaanishwa umechukulia kama kituko uonyeshe wenzako na hukujali kuhusu wao. Pole kwa kutambua ila jitahidi kuchukua hatua bora na njema pale inapohitajika

Tina Ndonde said...

uuwwiii usikute wana-abyuziwa huko kwa maboss wao na mpaka wameshazoea jamani, maana wazungu nao wanavitabia vya ajabu flani, sasa usikute hao mabeki tatu ndio wanavyofanyiwa hata wakiwa kwao....na wanaogopa kusema kisa wasipoteze ajira......uuwwiii Jide mimi nilivyokua mdadisi ningejitahidi mpk niulize mmoja wa hao wazungu.....mweeh ila km ni desturi na mila zao ni kabila gani tz wana mila na desturi hizo?? bado najiuliza...

Somebody Not Hater:... said...

Ubaya wa wbongo,wakiambiwa kitu tu wanadhani wanachukiwa!..........i said that kama nnavyoweza kumwambia mtu yeyote nnaempenda!...like a friend, sister or just anyone for yo info:.....I AM A JAYDEE'S NO. 1 FAN...AM NOT HATING AM JUST SAYING!.....TO U Suzan.

Disminder orig baby said...

Very sad!!
Hao managers lazima kuna kitu walijua, kwa nini hawakuwapa chakula katika vyombo kama vya wenzao? lazima kuna taarifa walipewa maybe!!!!

Inasikitisha sana, na hasa limetokea kwa rangi hii, imeniuma sana coz tunazidi kudharaulika, mila hizo? labda yote kheri

Anonymous said...

Du!!!!!!!!!!!! me shangaa sana ila nashindwa kuelewa kuwa ni tamaduni zao au la! ila mama kama ungekuwa umepalugha wanayo ongea au wametokea pande zipi katika nchi yetu au africa kidogo ingetupa mwanga kujua kama ni asili yao au ndo kama alivyo sema Subi au mchangiaji mwaingine kuwa wamefunzwa kwa kufananishwa na wanyama. Duniani kuna mambo!!!!!!!!!!!!!

Anonymous said...

SIS

Anonymous said...

jide hao watu wapo kwenye somo la kuwa waganga wa kienyeji, i mean wanasomea uganga wa kienyeji. so hizo ndo taratibu zao na desturi, kwa mfano wakiwa wameona wanasalimiana na kwa mmoja wao kuinama chini na kupiga magoti,waganga wa kienyeji watarajiwa hao.

Dorry said...

Hawa wazungu huwa wanapenda kutafuta entertainment huenda hio kwao ni kujifurahisha kupitia kwa wenzao!!!!tembea uone thanks Jide kwa kutusafirisha na sie kwa picha

mama C. said...

Hao watu walikua wanaongea lugha gani? au walikua kimya tu muda wote?? ila cha ajabu wana chezea simu so ni watu wenye akili zao... mmmmh hiyo mila ni kubwa kuliko!! hata kama ni research duh... sijui watalipwa bei gani maana kudhalilishana kwa hivyo big NO.

Rida said...

ila naona walitaka kufikisha ujumbe flani, kwa maana naona hata kutumia simu wanaonekana kma wanjua. je ukupata wasaa wakuongea nao?

Anonymous said...

Kuna biashara ya bin-adam siku hizi isije kuwa walikuwa wamenunuliwa na wanajaribu kuonyesha utii kwa wamiliki wao.Watu hudanganywa wanapelekwa ulaya na america kupewa makazi mazuri,kazi nzuri naahadi nyingi lakini inakuwa tofauti.
Mimi nauliza hao watu walikuwa humo Tanzania au ni nchi jirani au nje ya tanzania.
Na je ? kwa ufahamu wako ikiwa unawatilia shaka kiasi hicho uliweza kuvitaalifu vyombo vya usalama labda vingefuatilia kujua kulikoni.kwani wewe waweza kuogopa lakini wao watu au vyombo vya usalama vinaweza kuuliza na kupatiwa majibuna kama hawataridhika watawachukua kituoni kwa mahojiano zaidi,ikiwamo hata picha zao au alama za vidole kuwabaini ni akina nani na wanafanya nini,utaratibu huo unaweza ku rise flag inyoweza kuokoa maisha ya hao wamatumbi wenzetu.
Ni maoni binafsi.

cally said...

nionavyo hapo sio Tz wala EAST AFRICA ni SA..

Anonymous said...

i thin....ata hao waliokua nao lazima wanalifahamu hilo kitambo na inawezekana wamekua na hao ndugu zao kwa muda mrefu na walisha waambia kuhusu mila zao so hakuna mbaya kikubwa hawakulazimishwa kufanya hivyo, pia dada yangu J inawezekana ni kweli ni jambo geni kidogo but kwako limekua geni zaidi kutokana na utofauti wa mila zetu na zao.....sina tatizo namtuuuuuuu. yunus

Anonymous said...

kama ni south afrika nadhani itakuwa prank Jide ungusubiri uone mwisho wake iakuaje. kuna moja niliona cape town walikuja wale waafirica wanaofanana kama wale wa God must be cray kati kati ya eneo la wazungu beach area wakaanza kuchimba basi wazungu wakaanza kuwajia juu kuwatukana lkn wao waliendelea na kuonysha kibali kuwa ile sehemu ni yao na wamemilikishwa na Queen Magreth ilikuwa patashika wazungu walikuja juu ugomvi mkubwa lkn wale waafrika hawakujali walisisitiza kuwa ardhi ni yao na wakaendelea kuchimba. baadae kabisa ndio ikajulikana ilikuwa ni prunked. sijui nisemeje kiswahili msaada na spelling pia sina uhakika nazo. walitka kuona reaction ya watu itakuaje. sasa hapa inaokana kabisa ni kuigiza.

Anonymous said...

Jide hiyo ni acting tu mama ili kuona reation ya watu wengine itakuaje kuhusiana na maswala ya ubaguzi wa rangi, ukitka kujua hilo hata hiyo mito ilikuwa imetayarishwa kwa ajili yao na hat hizo tray za chakula. kama ingekuwa ni kweli basi wangekaa kwenye sakafu na sio kuomba mito au wangeeomba vigoda ambavyo ndio viti vya asili. kama ulivyosema kila kitu kilikuwa kimetayarishwa na hata hao wazungu waliokuja nao walikuwa hawajali lolote wala kushangaa wakisubiri reaction yenu mliokua hapo. vipingi kama hivi ni nimeviona vingi South Africa. reaction yenu ndo ingewafanya muujue ukweli. hao watu kama wangekuwa ni washamba kiasi hicho wasingeweza hata kuvaa nguo wala kutmia simu.

mama C. said...

Jide kwa hili umetuacha na maswali mengi zaidi ya majibu!! hebu rudi tena hapo restaurant kaulizie then utupe part 2 ya hiki kituko, Me mbea eeeh hahahahaha... ...kama alivyosema Disminder kuna kitu hapo restaurant wanakijua ndio maana walihudumiwa accordingly.

Anonymous said...

jIDE HILO KABILA LIPO Swaziland, na SA pia. Wabishi hao.... Usipime!
Ukiwaangalia wanachat kwenye simu zao, wanajua kila kitu, basi tu show off....
Lakini resercah siku hizi zinafanywa tofauti saana! Practical kwa saana kuliko theory. Utakuta wazungu hao wanapiga PHD zao huko za cultural shock, sisi tunabaki kushangaa...

JEN said...

HAHAHAHAHA WAMANG'ATI HAOO

Anonymous said...

Hapo Jide umeniacha kidogo umesema walikuwa wanakula kama wanyama mara walikuwa wanatumia mikono. Ila du kwanini wao wawekwewe kwenye sahani za mbao??

Anonymous said...

hao ni misukule

Anonymous said...

Hahhaha .misikitike sana..wanaekti .movie .sio Wazungu wte .wanatupenda.msg sent