Friday, July 20, 2012

KUTANA NA MBUNIFU MAVAZI AITWAE TASLEEM

Tasleem ni mbunifu wa mavazi na ana Kampuni yake inayojulikana kwa jina la Funeka, anatengeneza nguo na kuziuza sehemu mbali mbali kwenye maduka makubwa nchini Afrika Kusini
Mbali na hivyo Tasleem pia alikuwa na label yake ya nguo ambayo iko chini ya kampuni yake na mumewe "FUNEKA" ila ana mpango wa kuiua label hiyo ili abakie kushonea maduka makubwa na kuwauzia...
Label hiyo inajulikana kama SOUL CHILD
Tasleem mwenye umri wa miaka 39, amewahi kufanya kazi na duka la YDE "Young Designers Emporium" ambalo huuza nguo mchanganyiko za Local Deigners nchini humo..
Lakini kwa hivi sasa anafanya kazi na duka kubwa zaidi linalojulikana kama FOSCHINI ambako anawashonea nguo zinazokwenda kwa label yenye jina OASIS.

Quality ya vitambaa anavyotumia na finishing ni top of the line
Nimependa kufanya nae kazi, na atakua akinitengenezea nguo kadhaa, ambazo ni tofauti na zinazouzwa maduka ya FOSCHINI 
Bali kwa design za tofauti, tutakazo kuwa tukijadiliana mimi na yeye.
Kwani mbali na kuyashonea maduka makubwa anafanya kazi na wateja binafsi pia.

WIZI WA KAZI ZA SANAA:
Kama wanamuziki tunavyolalamika kuibiwa kazi zetu, wabunifu wa mitindo pia hulalamikia swala hilo.
Tasleem anakiri kuwapo wizi wa design za nguo zao hasa wanapokuwa wanafanya maonyesho ya kunadi kazi hizo. 
"FASHION SHOWZ"

Watu wengi wanazipenda lakini hawanunui, matokeo yake wanaishia kuzi copy na kuwapelekea mafundi wao wazitoe kama zilivyo.
Hivyo kuwasababishia ugumu katika soko

Ugumu huo anaoulalamikia mimi nimeuona nafuu
Ukilinganisha na ugumu wa soko la nchini kwetu.

Hivi Tanzania designer wanaweza wakashona nguo, wakaziuzia Boutique zaidi ya pieces hata 10 na zikapokea na kukubali kuuza Local Designs?????
Kama zipo labda mimi sijawahi kuziona!!! Mtanisamehe
Mimi navaaga Mustafa Hasanali, Farha Sultan na Khadija Mwanamboka kwa Tanzania...Sema wali maharage, mchicha, samaki daily? mara moja moja kuku, nyama, kisamvu n.k
Hapa tukioneshana michoro ya jinsi nguo nilizozichagua zitakavyokua.

Mbunifu huyo anakiri pia kuwa, designs mara nyingi hujirudia na mara zingine vionjo huweza kufanana...
Kwakuwa wabunifu wengi hubuni kutokana na kuchanganya designs zilizokwisha tengenezwa zamani.....Ila una pimp na kuongezea maujuzi yako sio kuiga kabisaaaa kama ilivyo ya mwenzako.......

Katika miziki inasemekana pia melody zimeisha, tunarudi mule mule, topic zenyewe pia ni zile zile kwani maisha tunayoishi pia yanakaribia kuwa yale yale....Yanatofautiana kidogo kuendana na wakati
Si vema nikiwaonyesha zile nilizonunua kiukweli hizi za kupigia picha tu for Blog, nilizozinunua mtaziona katika matukio muafaka.
Kila nikivaa nitaandika chini kuwa hii designed by Tasleem.
Kaa Macho!!!!
Well! Nyumba ya mwanamuziki hujaa ma guitar, vinanda na vingine vinavyofanana na hivyo.
Hali kadhalika nyumba ya designer wa nguo hujaa nguo na vitambaa, nyuzi, sindano, pini n.k

Hizi ni baadhi ya nguo zilizopo nyumbani kwake, ambazo nyingi huwa anazishona kwaajili ya maonyeho maalum ya siku moja tu na zote karibia ni size moja... 
Lucky me!!! zote zinanitosha
Kwakua ni model size, na huwa anashona zinazo mfiti yeye
Na hiyo size ndio size yangu mieeeee

Baada ya purukushani binti wa Mbibo huwa sijivungi, idara yangu hii

Hii ni moja ya nguo yenye nembo ya SOUL CHILD
Ukiona hako ka bichwa


4 comments:

cally said...

asante kwa kutujuza! nasubiri kuona atakazokushonea.

Somebody Not Hater:.... said...

Like the second picture from last......beautiful...love u JIDE!

Ester Ulaya said...

nasubiri kwa hamu kwakweli nione zitakavyokupendeza...nimependa mtiririko wa habari ulivyouweka

annette said...

naomba na mimi nipate size 18 tafadhali manake ata ile diet yako nilikuwaga na soma tu mwe!