NDUGU
zangu wanahabari, nimewaiteni leo kuzungumza nanyi kama mnavyofahamu
nawania nafasi ya Makamu Mwenyekiti wa klabu ya Yanga.
Nimejitosa
kuwania nafasi hii nikiamini nina uwezo na sababu ya kuiongoza Yanga,
ili niweze kutoa mchango wangu kwa klabu ninayoipenda tangu utotoni.
Ili
ndoto za yale ninayofikiri ni muhimu katika vipaumbele vyangu, kwa
kushirikiana na viongozi wenzangu sanjari na wanachama, kwanza kabisa
kutengeneza mfumo ambao mipango yake inatekelezeka.
Mfumo
huo wa awamu tatu tofauti, tukianzia mipango ya muda mfupi, muda wa
kati na mipango ya muda mrefu, ambao hata kama muda wetu wa kukaa
madarakani utamalizika, itawawia rahisi viongozi wajao kuongoza kwa
kufuata mfumo zaidi ambao utarahisiha utekelezaji wa majukumu yao.
Kama nikipata ridhaa ya kuiongoza Yanga kuna mambo ambayo nitayapa kipaumbele ikiwemo suala la marekebisho ya Katiba.
Kwa kushirikiana na viongozi wenzangu,
lakini kwa kuwashirikisha zaidi wanachama tutaipitia upya Katiba na
kuifanyia marekebisho, ili tuwe na Katiba imara, yenye nguvu
itakayoletea tija.
Kwa sasa Yanga haina dira wala mwelekeo.
Tunahitaji kuwa na dira na mwelekeo, bila hivyo hatutafika popote,
hivyo nikiingia madarakani kwa kushirikiana na viongozi wenzangu mtazamo
wangu utakuwa katika kujenga mfumo wa kudumu katika masuala yafuatayo.
(1) Umoja:
Kusimamia suala la umoja na mshikamano ndani ya klabu na kuondoa
makundi na kuhakikisha Yanga inakuwa moja kwani haiwezekani mwana- Yanga
adui yake, awe mwana Yanga, hivyo umefika wakati mambo hayo yaondolewe.
Ili
kuimarisha uhusiano na kujenga umoja ndani ya Yanga, tutahakikisha
vikundi vyote vilivyomo ndani ya klabu vinatambuliwa kikatiba ili viweze
kuendelea kuisaidia klabu kwa utaratibu ulio rasmi.
Hii
nikimaanisha viongozi wa matawi Tanzania nzima, Wazee, vijana na hata
vikundi vya ushangiliaji vinavyoleta hamasa katika michezo yetu
mbalimbali.
(2) Soka la vijana: Nitahakikisha natilia mkazo kuendeleza soka la vijana na kuibua vipaji vipya kama ilivyokuwa miaka ya zamani.
Mpira
si kama paa la nyumba kwamba siku zote linakuwa juu tu, soka inaanza
chini hivyo ni vyema watu wakatambua hilo, ili mchezo huu upige hatua
kama zilivyo nchi zilizoendelea duniani, ni lazima utengenezwe msingi
kwanza kwa kuchagua vijana wadogo, ambao baadaye watakuwa hazina kwa Yanga.
(3) SACCOS-
Kuwafanya wana Yanga wajivunie zaidi klabu yao, tutapanua wigo wa
taasisi yetu, kwa kuanzisha Mfuko wa Akiba na Mikopo kwa wanachama
(SACCOS), ambao utakuwa ukitoa mikopo kwa wanachama wake, kupitia matawi
jambo ambalo litaondoa utegemezi katika klabu na hata miongoni mwa
wanachama.
(4) KUJITEGEMEA:
Tutabadili mfumo wa uendeshaji klabu uendane na hali ilivyo ya soka la
sasa, ambapo klabu inatakiwa kujiendesha kibiashara, kwani Yanga ni
taasisi kubwa yenye fedha nyingi, ambazo zikitumika ipasavyo,
zitaisaidia timu kiuchumi na kujiendesha kisasa na jambo hilo
litawezekana iwapo tutakuwa na Katiba bora ambayo itawezesha jambo hilo
kutekelezeka kiurahisi.
Ni aibu klabu
kubwa kama Yanga kuwa maskini, wakati ina raslimali za kutosha ambazo
haziinufaishi, hivyo kubadili mfumo wa uendeshaji kutaifanya iweze
kujiendesha kwa kujitegemea.
Nia sio kurudi nyuma bali kwenda mbele na kuondoa umaskini uliokithiri
katika klabu yetu na kuifanya ijiendeshe kisasa na kuwa klabu ya kulipwa
ambayo inaweza kukabiliana na klabu nyingi kubwa za Afrika.
Kwa
kushirikiana na viongozi wenzangu nitaweka mawazo ya kuifanya Yanga
iweze kujiendesha kibiashara na ikiwezekana kubadili katiba kwa kutilia
mkazo suala la kampuni ili tuweze kuuza hisa za klabu, jambo ambalo
litasaidia kuongeza mapato pamoja na kuwajibika kwa wanachama ambao sasa
watakuwa sehemu ya klabu kwa karibu zaidi.
(5) UENDESHAJI WA KLABU: Pia katika kuboresha mfumo huu wa uendeshaji, tutaunda
idara kadhaa kwa ajili ya kurahisisha suala hilo, ambapo kutakuwa na
Idara za Uhasibu, Masoko, Sheria pamoja na ile ya Habari, Mawasiliano na
Uhusiano.
Pia shughuli zote zinazohusu klabu
zitafanyika makao makuu ya klabu yetu Jangwani, hivyo mawasiliano yoyote
ya kikazi baina ya wachezaji, viongozi, wanachama na wadau wa Yanga
yatafanyika klabuni lengo ni kuongeza heshima na uadilifu kwa Yanga.
Ili kulipa nguvu suala hilo tutalifanyia
ukarabati jengo la makao makuu ya klabu liwe na hadhi ya Yanga na kwa
ujumla uongozi wangu kwa kushirikiana na wenzangu utakuwa ule
unaozingatia zaidi Katiba.
(6) MATAWI:
Nitahahakikisha uongozi wangu unaimarisha matawi ya klabu na kufanya
wanachama kufahamu na kuchangia shughuli za klabu na kwa kuanzia itakuwa
busara kila wilaya zilizopo jijini Dar es Salaam kuwa na ofisi na
vitendea kazi muhimu na mpango huo utaendelea nchi nzima.
Lakini pia lazima niwe muwazi tangu
sasa, kuwa si kila jambo litahusisha wanachama wote, mfano mipango ya
timu kwa maana ya usajili, ushiriki wa ligi na michuano ya Kimataifa,
hilo likishikwa na watu wengi nafasi yake ya mafanikio huwa ndogo,
tutazipa nguvu kamati za ufundi na mashindano kufanya kazi kwa wepesi na
ushirikiano mkubwa.
KAULI YANGU KWA WANA-YANGA:
Naomba wanichague mimi wajenge imani
kwangu kwani nitahakikisha kwa kushirikiana na wenzangu tunajenga timu
imara ya ushindani, itakayokuwa tishio katika michuano ya ndani na ya
kimataifa. Wamchague Sanga kwa Yanga inayoeleweka.
SANGA KWA YANGA INAYOELEWEKA.
PICHA NA HABARI KA HISANI YA JOHN BUKUKU "Full Shang

1 comment:
Jamani article ndefu kusoma tu kaz!......
Post a Comment