Wednesday, June 19, 2013

SHUKRANI ZA DHATI KWA MAPENZI MLIOYAONYESHA TAR 14 JUNE 2013


Napenda kuchukua nafasi hii kutoa salaam zangu za shukrani kwa watanzania wote na wapenzi wa muziki kwa ujumla.
Kwa upendo na moyo mliouonyesha kuja ku support show yangu ya miaka 13 ya Lady JayDee pamoja na uzinduzi wa album ya Nothing but the truth.

Nilifarijika sana kuona umati mkubwa wa watu uliojitokeza bila kujali kuwa eneo lilikuwa limejaa
Nawaomba radhi pia kwa wale walioshindwa kuingia ndani.
Naamini yote hayo mliyafanya kutokana na mapenzi yenu ya dhati juu ya muziki huu.

Sina picha za ku post kwani picha zote zimesha postiwa kwenye blogs mbali mbali hapa nchini
Zaidi nitakuwa nafanya marudio tu ya ku copy paste, jambo ambalo si sawa kwa sasa.

Nawashukuru kwa kuzipokea nyimbo zangu zote mbili vizuri 1. JOTO HASIRA na 2. YAHAYA na kuziweka katika chart za juu kwenye radio stations zote ambazo hazina ubaguzi nchini Tanzania
Niwaahidi tu kuwa, nimerudi kazini rasmi na nitakuwa natoa kitu baada ya kitu.

Nitajitahidi pia kuendelea kuwa karibu nanyi, ili kupeana mawazo mbalimbali ya kujenga
Na pale kwenye mapungufu tushirikiane kurekebisha kwa pamoja.Kwa sasa nipo mjini NAIROBI - KENYA
kikazi kwa muda wa siku 5
Nitarejea Nyumbani Siku ya Ijumaa tuendelee na Sanya Sanya pale Nyumbani LoungeNikishamaliza kazi hii ilionileta, na nikiwa tayari nitawafahamisha ni kazi gani ila kwa sasa mta enjoy picha, Sina camera pia nimeisahau Dar.
Hivyo mvumilie kupata picha za simu yangu mbofu mbofu, ambazo hazina ubora wa hali ya juu

IJUMAA kuna Special appearance ya Patricia Hillary, muimbaji wa zamani ambae ndio alieimba original ya wimbo wa NJIWA peleka salamu.
Ni Nyumbani Lounge kuanzia saa 3:00 usiku
Lady JayDee na Machozi Band pia tutakuwa pamoja kuwapa burudani

Karibuni sana

16 comments:

Anonymous said...

ASANTE KWA SHUKRANI ZAKO NASIE TUNASHUKURU MUNGU ALITUPA UZIMA NA AFYA TUKAFIKA NA KUONA
TUTAENDELEA KUWA NAWE NA TUNAKUPENDA
MUNGU AWE NAWE NASI PIA

lyna wa ukweli said...

Shukran mamy pamoja sana.

Anonymous said...

una mpango wa kufanya show hapa nairobi..nambie tafadhali tupo hapa#team anaconda nairobi

nikita said...

Binafsi nimepokea shukrani. U did the greatest job....nakupenda bure tu...lets keep on doing what we do best...love u to the moon and back.

Anonymous said...

hongera saaaaaaaaana na pole na hekaheka za maandalizi ya miaka 13 sisi wa mikoan tulifurai sana kwa show ilivyopendeza usisahau kukonga nyoyo zetu watu wa mwanza

Anonymous said...

Nasi tunashukuru pia mama u did wonders keep it up....tupo nyuma yako always n forever...!ingawa sehemu ilikuwa ndogo iliwanyima watu wengne kukushuhudia...next time mama ufanye leaders ndio itakuwa freshhh...we lov u jide. Na mumeo pia as ur manager coz tulimuona alivyokuwa anajitahd kukarbisha wagen nakuzunguka sana kuonyesha kila kitu kinaenda acordingly...Salute

Anonymous said...

team anakonda hongereni sanaaaaaaaaa inabidi utuandalie shoo nyingine ya shukrani ikiwezekana eneo kubwa na sie tuliokua nje tuweze kujiachia.upo juuuuuuuuu na hauna mpinzani.

Not Hater; said...

All the best swily!!!!!!!!!!

Anonymous said...

Nimekubali "Strength of a Woman" nikupongeze pia kwa kupata mume anayekupa ushirikiano ambao ni wanaume wachache sn wanaweza hiyo wengi utasikia mke wangu yuko na biashara zake huko huku anaishia kunywa bia na friends

maggie bomoa. (team anaconda) said...

hasante kwa kushuru. maana ni wachache wanaojua kushukuru.

MissTeam Anaconda..Uk..bby said...

Hongera sana Anaconda kila kona hata huku wadau wako wa uk. Km vile tulikuwa bongo coz djchoka alikuwa anaturushia kilatukiyo kwa instagram...tulifuraije..maana hatutokaa tukadahau hiyo ck tulikesha pamoja sana..

Anonymous said...

Comando Anaconda, sherehe zilionyesha kwamba wengi wanayo kiu ya muziki wako, sasa wape wapenzi wako shukrani ya Tamasha Kubwa zaidi katika eneo litakalo chukua idadi kubwa ya watu. Iwe ni baada ya wewe kufanya utafiti wa gharama na idadi ya watu watakao ingia kwenye matamasha hayo.

NB: Ikiwezekana ufanye matamasha kwa kanda ama mikoa yote.

Ulichokianzisha kiendeleze.....

Disminder orig baby said...

Yeeeeeeeeeeeereerr
Wanawake juuuu

Anonymous said...

I love u jide

Anonymous said...

mungu akubariki na kukutangulia in any way

Anonymous said...

Thank you..endelea kuwakalisha lzm wakae!